.

RAIS WA ZAMANI WA CUBA, FIDEL CASTRO, AFARIKI DUNIA

Nov 26, 2016

Serikali ya Cuba imetangaza habari ya kufariki dunia Fidel Alejandro Castro Ruz, rais wa zamani wa nchi hiyo mapema leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 90.
Fidel Castro mbali na kuongoza mapinduzi nchini Cuba mwaka 1959 hadi 1976 alikuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, huku akishika nafasi ya urais tangu mwaka 1976 hadi mwaka 2008. Chama cha Kikomonisti ambacho ni chama pekee nchini Cuba kupitia mfumo wa chama kimoja, kilikuwa madarakani kuanzia mwaka 1965 hadi 2011 chini ya Castro mwenyewe.

Fidel Castro kuanzia ujana hadi uzeeni
Katika kipindi cha utawala wake, taifa la Cuba lilishuhudia ukuaji wa viwanda na biashara. Aidha rais huyo wa zamani wa Cuba anafahamika kama hasimu mkubwa wa Marekani ambaye kwa kipindi chote aliendesha mapambano makali ya kisiasa dhidi ya Marekani na hivyo kujipatia umashuhuri mkubwa duniani.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช