Na
Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muugano wa Tanzania imeishauri Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) kukaa meza moja na
nchi wanachama wa Mkataba wa Roma hususani
zile za Afrika ili kutafuta suluhu ya
changamoto na tofauti zilizopo kati ya mahakama hiyo
na wanachama wake.
Tanzania imetoa mwito huo siku ya jumatatu kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, wakati
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilipopokea na kujadili Taarifa ya Utendaji ya
Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.
Taarifa
ICC imewasilishwa na Rais
wa mahakama hiyo Jaji Slivia
Fernandez de Gumendi katika
kupindi ambacho Jumuiya ya Kimataifa imekumbwa
na taharuki baada ya
wanachama wawili wa Mkataba wa Roma, Afrika ya Kusini na Burundi kuwasilisha rasmi katika Umoja wa Mataifa kusudio la kujiondoa huku
Gambia nayo ikitangaza kutaka kujitoa ingawa bado haijawasilisha rasmi nia yake hiyo.
Mwakilishi huyo wa Tanzania katika mchango wake amesema, uwepo au kuanzishwa kwa ICC kulitokana kwa
kiasi kikubwa na uungwaji mkono kutoka Afrika.
Akasema uungwaji
mkono huo ulitokana hasa baada ya
nchi
hizo za Afrika kukatishwa tamaa
na kuvunjika moyo baada ya kutokea
kwa mauaji ya kimbari nchini
Rwanda.
“Baada
ya kukatishwa tamaa na kuvunjwa moyo, Mahakama
hii, ilikuja kuwa chombo cha
kutenda haki dhidi ya watu
waliojihusisha na vitendo vya kikatili
vikiwamo vya ukatili
dhidi ya binadamu, uhalifu kivita na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Madhira
yasiyoelezeka yaliyotokea Barani Afrika
yakaifanya mahakama hii kuwa chombo cha matumaini dhidi ya wale ambao hawakuweza kuguswa au walikuwa
juu ya sheria”. Akasema Balozi
Manongi
Na
kuongeza. “ Kama nchi mwanachama wa Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa
ya Jinai na Mwanachama wa Umoja wa Afrika. Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inatambua kwamba, uhusiano
kati ya mahakama na Afrika ni ule wa
misuguano, na ni uhusiano ambao
umeleta hofu ya Afrika kujitoa”.
Balozi
Tuvako Manongi akaeleza zaidi kwamba,
hofu hiyo ya kujitoa kwa Afrika katika
mahakama hiyo, haipaswi kuwepo kutokana na mambo
kadhaa ambayo Afrika
imejipanga kuyatekeleza kwa manufaa
ya bara hilo na watu wake.
Baadhi ya
mipango hiyo ni utekelezaji wa
ajenda ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika maarufu kama agenda 2063 ambayo pamoja na
mambo mengine inachagiza katika
utawala bora, demokrasia,
usawa wa jinsia, kuheshimu haki
za binadamu, haki na utawala wa sheria..
“Viongozi
wa wakuu wa nchi na serikali wa Afrika wameutangaza mwaka 2016 kuwa mwaka wa haki za binadamu huku mkazo ukielekezwa katika haki za wanawake.
Na katika kutambua kuwa Amani na Haki ni
vitu ambavyo haviwezi kutenganishwa, kwa
sababu hizo, tunachotakiwa kuhimiza leo sana sana ni majadiliano”.Akasisitiza Balozi.
Tanzania pia
ikaeleza kwamba ni vema Mahakama
hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake
ikajenga mazingira ya kuaminiana kati
yake na wanawachama wake.
Tanzania
pia kupitia Mwakilishi wake, imezitaka
nchi hususani zile za mataifa yaliyoendelea kuacha
kuzihubiria nchi zinazondelea kama vile zenyewe ni adilifu sana. Na kusisitiza kwamba, kinachotakiwa wakati
huu si kunyosheana vidole au
kulaumiana bali kufanya kazi kwa
pamoja ili kuifanya mahakama hiyo iendelee kutekeleza
majukumu yake kwa uwazi , haki na kuaminiwa.
Akasisitiza
pia kuwa hata kama matatizo yaliyopo
baina ya ICC na Africa yatapatiwa
ufumbuzi. Bado kuna haja na umuhimu kwa
nchi za Afrika kuziimarisha na kuzijengea uwezo Taasisi zake
na vyombo vinavosimamia utoaji wa haki na utawala wa sheria ili viweze kushughulikia makosa ya jinai yakiwamo ya ukatili dhidi ya binadamu na uhalifu wa
kivita badala ya kusubiri au kutegemea mahakama za kimataifa kama ICC.
Akabinisha kuwa
nchi zinatakiwa kuwajibika
kikamilifu siyo kwa kuhofia
kuingiliwa mambo yao ya ndani na ICC bali kwa sababu zinaowajibu wa kwanza wa kuwalinda raia wao.
“Kwa
Afrika matukio kama yale ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cote d’ Ivore, Rwanda na
Sierra-Leone ni kielelezo cha hatari
ambayo tunatakiwa kujikinga nayo.
Vile
vile Tanzania imelitaka Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa,
kutopeleka ICC rufaa zenye malengo
wa kisiasa kwani kwa kufanya hivyo
kunachangia kuharibu sifa ya ICC na kuifanya isiaminiwe na kuonekana inatumiwa
na wakubwa kutimiza malengo yao.
Pamoja
na kulitaka Baraza la Usalama kutoingiza siasa katika rufaa zake,
Tanzania pia imewashangaa baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo na ambao si
wanachama wa Mkataba wa Roma kuwa mstari wa mbele katika kupeleka rufaa kwenye Mahakama hiyo dhidi ya mataifa mengine.
Wazungumzaji
wote zaidi ya 50 walioomba kuchangia
Taarifa hiyo ya ICC pamoja na kuzungumzia utendaji kazi na changamoto zinazoikabili Mahakama hiyo, walijielekeza zaidi katika
kuelezea masikitiko yao juu ya
uamuzi wa Afrika ya Kusini na Burundi
kujitoa.
Wasemaji hao
kama ilivyokuwa kwa Tanzania walisisitiza sana umuhimu wapande zinazopingana kukaa mezani na kuzungumza huku baadhi yao wakizitaka
Afrika ya Kusini na Burundi
kufikiria upya uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269