Breaking News

Your Ad Spot

Nov 28, 2016

UGANDA : VURUGU ZAZUKA NA MFALME WA RWENZURURU AKAMATWA

media
Nchini Uganda, Mfalme wa Rwenzururu, Charles Mumbere, amekamatwa Jumapili hii tarehe 27 Novemba na atapelekwa katika mji mkuu, Kampala. Msemaji wa polisi anasema Mfalme huyo anashitakiwa kwa "uchochezi wa vurugu".
Kukamatwa huko kumetokana na kutokea kwa wimbi jipya la ghasia zilizoibuka wiki hii nchini Uganda, katika mkoa wa Rwenzori unaopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wakati wa makabiliano dhidi ya vikosi vya usalama vya Uganda, hali ilikua tete siku ya Jumamosi ambapo watu 55 waliuawa. Mvutano katika mkoa huo ulitokana na uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.
"Watu wengi walipoteza maisha katika makabiliano hayo. Polisi kumi na wanne waliuawa na washambuliaji 41 waliangamizwa ", polisi imesema Jumapili hii asubuhi katika mkutano na waandishi wa habari. Maafisa wengine wanne na askari wawili walijeruhiwa.
Wakati ambapo polisi na jeshi walikua wakipiga doria karibu na kasri ya Mfalme wa Rwenzururu asubuhi ya Jumamosi Novemba 26, "walinzi wa Mifalme walishambuliwa kikosi hicho,"amesema msemaji wa polisi, Felix Kaweesi.
Mashambulizi mengine yalitokea katika mkoa huo na gari la polisi lilichomwa moto. Kwa mujibu wa polisi, mashambulizi haya yalikuwa "yaliandaliwa vizuri" na washambuliaji walikua na vifaa vya kutosha ikiwa ni pamoja na 'bunduki' na 'mabomu.'
Kama hakuna uhusiano wowote ambao utathibitishwa moja kwa moja kuwa ni waasi wa mashariki mwa DRC walioendesha mashambulizi haya, pengine litakua kundi la waasi wa Uganda wa ADF. Polisi bado inashuku uwezekano wa kuwepo kwa mawasiliano hasa kwa kubadilishana silaha.
Sababu ya vurugu hizi mpya inaonekana kuwa ni ya kisiasa na inahusishwa na nia ya kuunda eneo huru nchini Uganda, Jamhuri ya Yiira.RFI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages