.

AJALI YA LORI LA MAFUTA YAUA WASIOPUNGUA 25 NCHINI KENYA

Dec 11, 2016

Mripuko wa lori lililobeba shehena ya mafuta katika barabara moja kuu nchini Kenya umeua watu wasiopungua 25.
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo eneo la kilomita 10 kaskazini mwa mji wa Naivasha ulioko katika mkoa wa Bonde la Ufa katikati mwa Kenya.
Akizungumza kutoka eneo la tukio, afisa wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu Felister Kioko amesema: "Hadi sasa tumekusanya maiti 25 kutoka eneo la tukio la ajali baada ya lori lililokuwa likielekea Uganda kupoteza udhibiti na kugonga magari mengine kadhaa."
Ajali ya lori la mafuta
Itakumbukwa kuwa mwaka 2009 zaidi ya watu 100 waliungua hadi kufa karibu na mji wa Molo ulioko katikakati mwa Kenya pia baada ya lori lililobeba shehena ya mafuta ya petroli kuwaka moto.../ 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช