.

MHARIRI WA HABARI MSTAAFU WA MAGAZETI YA UHURU, MZEE NAKAJUMO ATINGA NEWSROOM LEO KUWANOA VIJANA

Dec 7, 2016

 Mhariri wa Habari Mstaafu wa Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru Mzalendo na Burudani Mzee Joe Nakajumo akimpiga msasa Kaimu Mhariri wa Makala Selina Wilson, katika chumba cha habari cha kampuni hiyo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Mzee Nakajumo alifika leo katika chumba cha habari kwa mwaliko rasmi wa Kaim Mhariri Mtendaji wa UPL, Ramadhani Mkoma ili kuwapiga msasa waandishi wa habari. Kulia ni Mpigapicha Mwandamizi wa UPL, Bashir Nkoromo ambaye kwa sasa ameazimwa Katika Idara ya Itikadi na Uenezi, Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Makao Makuu ya CCM.
 Kaimu Mhariri wa Makala, Selina Wilson akimshukuru Mzee Nakajumo kwa msasa aliompiga
 Mpigapicha Mwandamizi wa UPL, Bashir Nkoromo ambaye kwa sasa ameazimwa Katika Idara ya Itikadi na Uenezi, Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Makao Makuu ya CCM, akimshukuru Mzee Nakajumo baada na yeye kupata nasaha na kukumbushwa namna kazi zilivyokuwa zikifanyika wakati akipigapicha UPL ambapo picha zilikuwa lazima zitathminiwe ubora  wake na Mzee huyo, Nakajumo wakati akiwa bado hajastaafu UPL
Mzee Nakajumo akiendelea kusikiliza kila liyetaja kulifahamu kwa undani jambo linalohusu uandishi wa habari ulio wa makini zaidi. PICHA ZOTE NA JUMAANE GUDE

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª