.

MASAUNI ATEMBELEA MAGEREZA UKONGA,AJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOFANYWA NA JESHI HILO

Jan 4, 2017

 Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa na Mkuu wa Magereza kamishna Juma Malewa akizungumza  jambo na waanddishi wa habari katika gereza la Ukonga Jijini Dar es salaam.
 .Naibu Waziri  wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na  Mratibu wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza Bw. Julious Chege  katika gereza hilo la Ukonga,jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na Kaimu kamishna wa Jeshi la Magereza Juma Malewa mara baada ya kukagua Kiwanda cha kutengeneza Samani Katika gereza la Ukonga.
 Na Anthony John Glob Jamii.

NAIBU Waziri  mambo ya Ndani  Mhandisi Hamad Masauni amelitaka jeshi la zimamoto na  Uhamiaji kutoshona sare zao za uraiani, badala yake wakashone katika jeshi  la Magereza ili kubana matumizi ya serikali.
Masauni ameyasema hayo  leo katika  ziara yake ya kutembelea  Magereza Ukonga,jijini Dar, ambapo amekagua  Kiwanda  cha Magereza kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na nguo za askari Magereza.
Sanjari na hayo Mhandisi Masauni ametoa wito  kwa Watanzania kwa kununua  bidhaa mbali mbali zinazo tengenezwa na jesi la Magereza ili kuunga mkono kwa kazi nzuri wanazozifanya.
Aidha amewapongeza askari wa jeshi la  Magereza kwa kujitolea kujenga nyumba zao bila kusubiri serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali itaandaa bajeti Mwakani ili kumalizia maeneo machache yaliyo baki.
Naye   kaimu Mkuu wa Magereza  Kamishina Msaidizi . Juma Malewa amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi  kama mashine za  kushonea nguo, na mashine za za ufundi selemala , ukosefu wa mtaji wa kuendesha shughuli za kilimo,  hivyo amesema pindi serikali itakapo wawezesha watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª