Breaking News

Your Ad Spot

Jan 29, 2017

RAIS DK. MAGUFULI AHUDHURIA KIKAO CHA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA, LEO

Ikulu, Dar es Salaam
Rais wa Dk. John Magufuli, leo Januari 29, 2017 ameanza kuhudhuria mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, leo asubuhi  Dk. Magufuli amehudhuria mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Chad Idriss Deby Itno ambapo wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanakutana na Katibu Mkuu Mpya wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres.

Imefanua taarifa hiyo kuwa, madhumuni ya mkutano huo ni kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uhusisano kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, hususani katika kuimarisha masuala ya amani na usalama.

"Mkutano huo utafuatiwa na mkutano maalum wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika utakaoongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Mhe. Idriss Deby Itno", imesema taarifa hiyo ya Ikulu.

Taarifa imeongeza kuwa Rais Magufuli pia atahudhuria chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika (AUC) Mhe. Dk. Nkosazana Dlamini Zuma kwa lengo la kutangaza rasmi jina la kituo kipya cha amani na usalama ambacho kimepewa jina la Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni kutambua mchango wake katika kupigania amani na usalama wa Afrika.

Kituo hicho kipo ndani ya majengo ya makao makuu ya Umoja wa Afrika Mjini Addis Ababa na Rais Magufuli atatoa hotuba fupi mara baada ya kukitangaza rasmi.
Rais Dk. John Magufuli akiteta jambo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyattaa kwenye mkutano huo, leo asubuhi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages