Breaking News

Your Ad Spot

Jan 30, 2017

ZIARA YA KIKAZI YA NAIBU WAZIRI MASAUNI MKOANI KATAVI

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando wakati akiwasili ofisi ya mkoa huo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za  masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa  serikali mkoani hapo.

 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando (kushoto), akitoa taarifa ya Mkoa  kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya  Naibu Waziri huyo mkoani hapo ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi
 Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Paul Chagonja akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo  mkoani hapo yenye  lengo la kuona changamoto za  masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wakwanza kulia), akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo  mkoani hapo kwa  lengo la kuona changamoto za  masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa mkoa huo kutoka kada mbalimbali
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia),akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando,(wapili kulia). Naibu Waziri alifika mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi. Wengine ni viongozi wa mkoa huo kutoka kada mbalimbali (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages