WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema hata kwa
goli la mkono ni lazima Serengeti Boys warejee nyumbani wakiwa ama na
kombe au wakiwa wamefuzu kushiriki kombe la dunia kuwa moja ya timu
mbili zinazohitajika.
Kauli ya Waziri Nape ameitoa leo asubuhi wakati akifungua mashindano ya
Kombe la Standard Chartered 2017 safari kuelekea Anfield ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917
yaliyoanza kutimua vumbi katika viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu,
Gerezani.
Alisema haiwezekani taifa hili kuwa na Waziri mjanja kama Nape halafu
Serengeti Boys inakosa kombe huko Gabon na nafasi ya ushiriki Kombe la
dunia.
Pamoja na kauli yake hiyo Waziri Nape aliiomba Benki ya Standard
Chartered kushiriki katika jukumu la kuhakikisha kwamba Serengeti Boys
ama inarejea na kombe au inafuzu miongoni mwa timu mbili zitakazoshiriki
Kombe la Dunia.
Picha
juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye (katikati), Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered,
Tanzania Sanjay Rughani (wa tano kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya
uamuzi TFF, Salum Chama (wa tatu kulia) wakijumuika kwa pamoja na
washiriki wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to
Anfield) kutoka makampuni mbalimbali kupasha misuli moto yaliyoanza
kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani
jijini Dar es Salaam.(Picha na thebeautytz.co.tz)
Alisema kwa sasa serikali inawaomba wadau kushiriki katika kuhakikisha
kwamba Kambi ya Serengeti Boys inaimarika na kuwezesha kuwa na kikosi
cha ushindi.
Aliishukuru Benki hiyo kwa kuhakikisha kwamba inainua michezo nchini kwa
kusaidia kunyanyua na timu ya wanawake na kusema kitendo cha wao
kuileta Dunia nchini Tanzania (Liverpool na mashabiki wake na michuano
ya kuelekea Anfield) ni cha kushukuriwa sana.
Aliishukuru pia kwa kumleta nguli John Barnes na kulitaka Shirikisho la
kabumbu nchini (TFF) kuhakikisha kwamba wanatumia nafasi hiyo kuwaweka
sawa pia kisaikolojia vijana wa Serengeti Boys.
Alisema ujio wa Barnes unaneema kubwa hasa ratiba yake ya kukutana na
vijana wa Serengeti.
Pamoja na kuzungumzia Serengeti Boys, Waziri Nape aliitaka jamii
kuthamini michezo na kushiriki kwa kuwa huleta afya na kujenga umoja.
Alitaka timu zote 32 zinazowania kufuzu kucheza ngwe ya Afrika mashariki
kucheza kwa bidii na furaha na kuhakikisha wanapata ushindi halali ili
waweze kuiwakilisha vyema Tanzania katika michuano ya Afrika Mashariki
jumamosi ijayo.
Washindi wa mwaka jana timu ya Mwananchi ilitolewa mapema katika
mashindano hayo ambayo yanaendelea hadi jioni ya leo wakati mshindi
atakapopatikana.
Mshindi wa mashindano hayo atapambana na washindi kutoka Kenya na Uganda
ambao nao leo wanawasaka washindi wao katika nchi hizo.

Pamoja na kuzungumzia Serengeti Boys, Waziri Nape aliitaka jamii
kuthamini michezo na kushiriki kwa kuwa huleta afya na kujenga umoja.
Alitaka timu zote 32 zinazowania kufuzu kucheza ngwe ya Afrika mashariki
kucheza kwa bidii na furaha na kuhakikisha wanapata ushindi halali ili
waweze kuiwakilisha vyema Tanzania katika michuano ya Afrika Mashariki
jumamosi ijayo.
Washindi wa mwaka jana timu ya Mwananchi ilitolewa mapema katika
mashindano hayo ambayo yanaendelea hadi jioni ya leo wakati mshindi
atakapopatikana.
Mshindi wa mashindano hayo atapambana na washindi kutoka Kenya na Uganda
ambao nao leo wanawasaka washindi wao katika nchi hizo.

Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati),
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani
(mwenye kofia) na Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama
(kushoto kwa Waziri Nape) katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi
bendera kwa washiriki kutoka makampuni mbalimbali wa mashindano ya Kombe
la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917
yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo
Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Zawadi ya timu itakayoshinda Afrika Mashariki ni safari ya kwenda
Liverpool na kuangalia mechi zitakazpigwa na timu hiyo katika uwanja wa
Anfield mwezi Mei.
Aidha timu hiyo itapata nafasi ya kutembelea uwanja wa Anfield na
kukutana na magwiji mbalimbali wa Liverpool.
Safari hiyo ya timu ya watu saba italipiwa na Benki ya Standard
Chartered ambayo inafadhili timu ya Liverpool yenye mashabiki zaidi ya
milioni 700 duniani.


Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani akisoma
risala kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
(hayupo pichani) wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered
2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100
tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo
kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es
Salaam.
Awali Mwenyekiti wa waamuzi Salum Umange Chama ambaye alimwakilisha Rais
wa TFF Jamal Malinzi aliishukuru benki ya Standard kwa kuwa championi
wa michezo na kwa kufadhili mafunzo ya wamuuzi na timu ya wanawake.
Aliitaka Benki hiyo kuendelea kufadhili michezo nchini ili iweze kukua.
Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania
Sanjay Rughani Sanjay amesema kwamba benki yake inaona fahari kuwa mgeni
wa michuano hiyo kuelekea Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki na
kuwataka washiriki wakaze nia ya kutwaa ubingwa.
Alisema mashindano ya mwaka huu yanaendana na miaka 100 ya shughuli za
benki hiyo nchini Tanzania.


Mwenyekiti
wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Nape Nnauye kubariki mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017
(Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu
benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye
viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Pia alisema anaona fahari kuwapeleka washindi kuzuru uwanja wa
kihistoria wa Anfield na kuwatembelea Liverpool FC timu iliyoanzishwa
1892 nchini Uingereza hadi kwa wananchi wa kawaida kwa kuanzisha
mashindano hayo ambapo timu inacheza kwa dakika 10 ikiwa na wachezaji
watano na wawili wa akiba.
Mashindano hayo yapo katika bara zote ambapo benki ya Standard
Chartered inafanyakazi.


Mgeni
rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
akizungumza na washiriki wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered
2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100
tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo
kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es
Salaam.


Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati)
akibadilishana mawazo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered,
Tanzania Sanjay Rughani wakati mashindano ya Kombe la Standard Chartered
2017 (Road to Anfield) yakiendelea katika viwanja vya JK Park Kidongo
Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati
ya uamuzi TFF, Salum Chama.

Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizundua rasmi
mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari kuelekea Anfield
kwa kupiga mpira kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani
jijini Dar es Salaam.

Mchezaji
wa Benki ya Standard Chartered (jezi nyeupe) akichuana vikali na
wenyeji wa JK Park (jezi za kijani) kwenye mechi ya kwanza ya dakika
kumi wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 ya safari
kuelekea Anfield ambapo timu ya JK Park iliibuka kidedea kwa bao 1-0.


Mchezaji
wa Mwananchi Communication (tisheti nyeupe) akijaribu kumtoka mchezaji
wa ORYX kwenye wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari
kuelekea Anfield ambapo timu ya ORYX Park iliibuka kidedea kwa bao 2-0.

Mshehereshaji
wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield),
Maulid Baraka wa Kitenge (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Miradi
wa Executive Solutions, Hilda Ngowi (katikati) na Mhasibu wa Executive
Solutions, Mapunda (kushoto) wakati wa mashindano ya Kombe la Standard
Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi
leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es
Salaam.

Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa kitengo cha makampuni makubwa wa benki
hiyo, Jaffer Machano wakati wa mashindano ya Kombe la Standard
Chartered 2017 (Road to Anfield) ) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua
vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini
Dar es Salaam.

Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) kwenye
picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered,
Tanzania Sanjay Rughani (wa pili kushoto), Mkuu wa kitengo cha makampuni
makubwa wa benki hiyo, Jaffer Machano (wa pili kulia), Mwenyekiti wa
Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama (kulia) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko
wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) wakati
mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka
1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo
Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269