.

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AMJULIA HALI MKURUGENZI WA TEHAMA

Feb 3, 2017

Daktari Bingwa Upasuaji wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Nicephorus Rutabasibwa (kulia) akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge Job Ndugai  (wa tatu kushoto) Dar es Salaam jana wakati alipofika kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT)  wa Bunge, Lily Mraba aliyelazwa katika Taasisi hiyo
 Muuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Zaituni Bembe (kushoto) akiagana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai  Dar es Salaam jana mara baada ya kutoka katika Taasisi hiyo, wakati alipokwenda kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT) wa Bunge, Lily Mraba.
Daktari wa Mishipa ya Fahamu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)  Hamisi Kinyerero (kulia) akiagana na maofisa wa Bunge walioongozana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai wakati alipofika kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT) wa Bunge, Lily Mraba. aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa MOI. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA )

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช