Na Edwin Moshi wa Eddy Blog
Lori
lililokuwa limebeba mawe limepinduka katika kijiji cha Masisiwe
wilayani Makete na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa katika
lori hilo.
Taarifa
za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa lori hilo limepoteza
muelekeo ghafla kisha likaanza kupinduka kwa kubiringika mara kadhaa
umbali unaokadiriwa kuwa zaidi ya mita 80 kutoka barabarani. Ajali hiyo inadaiwa kutokea kati ya saa nane na saa tisa alasiri hii jana.
Baadhi
ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ambao hawakutaka kutaja majina yao
wamesema Lori hilo lilikuwa linatoka kubeba mawe kwa ajili ya kujenga
daraja katika kata ya Ipepo kabla ya kupoteza mwelekeo likiwa njiani na
kupinduka kisha kuporomokea bondeni.
Jeshi la polisi Makete limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi. Tutawaletea taarifa kamili ya tukio hilo pindi mamlaka husika zitakapatia.
Polisi wakipima jinsi ajali hiyo ilivyotokea
Askari Polisi akiangalia mawe yaliyokuwa yamebebwa na lori hilo kabla ya kutokea ajali
Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari la polisi
Lori hilo likionekana kwa mbali baada ya ajali
Muonekano wa lori hilo baada ya ajali
Ajali ilipoanzia, hapa ndipo lori hilo lilipotumbukia
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269