.

BASI LA RUKSA CLASSIC LAGONGANA USO KWA USO NA GARI DOGO SHINYANGA

Mar 14, 2017

Basi la RUKSA CLASSIC lenye namba za usajiri T 636 AWC likitoka jijini Mwanza kwenda mkoani Kigoma limegongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajiri T 210 DJJ katika kijiji cha Nhelegani mkabala na chuo cha Ushirika Moshi kambi ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.

Chanzo cha ajali hiyo kimeeleza kuwa ajali hiyo   iliyotokea majira saa nne asubuhi ni uzembe wa dereva wa gari ndogo ambaye hakuwa na utulivu barabarani na kujikuta yupo upande wa usiokuwa wake na kujikuta kugongana uso kwa uso na kusababisha ajali hiyo.

Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa dereva wa gari dogo na abiria wake mmoja, wameumia na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa gari dogo kufuatia ajali hiyo

Muonekano wa basi kufuatia ajali hiyo. (PICHA ZOTE NA MASENGWA BLOG)
Muonekano kwa Nyuma ya gari dogo

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช