Breaking News

Your Ad Spot

Mar 27, 2017

MADAKTARI BINGWA WA MOYO KUTOKA HOSPITALI YA SAIFEE YA INDIA NA WENZAO WA JKCI WAFANYA UPASUAJI KWA WAGINJWA


Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari  wa Hospitali ya Saifee ya nchini India wakimfanyia upasuaji mgonjwa anayesumbuliwa na tatizo la moyo leo Machi 27, 2017. Baada ziara aliyoifanya nchini mwishoni  mwaka jana kiongozi Mkuu wa Madheebu ya Bohora Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal Saifuddin alimuahidi Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuleta madaktari wa Moyo nchini ambao watashirikiana na Madaktari wa JKCI kufanya upasuaji kwa wagonjwa. Timu ya  wataalam hao ambao idadi yao ni sita  imeshawasili nchini na tayari wameanza kufanya upasuaji ambao utachukuwa  siku tano na wanatarajia kufanya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba  ( CABG-Coronary Artery Bypass Graft) na upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo inamatatizo na inahitaji kubadilishwa kwa wagonjwa 15. (PICHA NA ANNA NKINDA-JKCI)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages