Breaking News

Your Ad Spot

Mar 15, 2017

MAZISHI YA SIR GEORGE KAHAMA KUFANYIKA KESHO, SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA ATOA POLE KWA WAFIWA

 Marehemu Sir George Kahama enzi za uhai wake.
 Spika Mstaafu, Anne Makinda akisaini katika kitabu cha maombolezo cha Sir George Kahama nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
 Spika Mstaafu, Anne Makinda akimfariji mjane wa marehemu Janeth Kahama.
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sofia Simba akimpa pole mjane wa marehemu, Janeth Kahama.


Mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Regina Lowassa (wa pili kulia), akiwa kwenye msiba huo.
 Sophia Simba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bakari Mwapachu katika msiba huo.
 Pole zikiendelea kutolewa kwa mjane wa marehemu.
Waombolezaji wakiwa msibani.

Na Dotto Mwaibale

MAZISHI ya aliyekuwa Waziri na Mwanasiasa Mkongwe Sir George Kahama yanatarajiwa kufanyika kesho kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mwili  wa marehemu utawasili nyumbani kwake eneo la Mikocheni B kituo cha mabasi kijulikanacho kama Business leo hii saa 11 jioni na kukesha hadi asubuhi.

Kesho mwili wa marehemu  utaondolewa nyumbani kwake kuelekea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia  saa mbili kamili kwa ajili ya viongozi mbalimbali na wananchi kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuelekea Kanisa la Mtakatifu Petro ( St. Peters) Oysterbay Dar es salaam saa tano nanusu 5.30 asubuhi kwa ibada.

Ibada ya mazishi  itafanyika  katika  makaburi  ya Kinondoni kuanzia saa tisa na nusu  9.30 alasiri.


1 comment:

  1. Condolences to the Kahama family and friends. May Sir George Rest in Peace.

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages