.

MKUTANO KUU MAALUM WA CCM WAFANA DODOMA, LEO, WAJUMBE WAPITISHA KWA KISHINDO KATIBA MPYA YA CHAMA

Mar 12, 2017

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasili ukumbini tayari kuendesha Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mstaafu na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu John Malecela, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangu na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasili ukumbini tayari kuendesha Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, mjini Dodoma leo. Kushoto Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM mstaafu na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu John Malecela, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangu na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
 Baadhi ya viongozi wastaafu katika nafasi mbalimbali wakiwa wamewasili ukumbini
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika leo katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akimsifuMwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa CCM uliokuwa ukiitwa Dodoma Convertion Centre ambapo baada ya sifa hizo, Dk Mafuguli aliwaomba wajumbe kukubali pendekezo lake la kutaka ukumbi huo sasa ujulikane kwa jina la Jakaya Kikwete ambapo wajumbe hao waliafiki
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa maelezo kuhusu mabadiliko yanayotakuwa kupitishwa na Wajumbe wa mkutano huo. 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimshauri jambo Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli wakati wa mkutano huo
 Mwimbaji wa taarab na kwaya wa TOT, Khadija Kopa akiimba wakati kundi hilo lilipotumbuiza wakati wa mkutano huo, leo
 Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole akitoa maelezo ya kutambulisha wageni mbalimbali wakati wa mkutano huo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo akiwa ukumbini wakati wa mkutano huo. Kushoto ni aliyekuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Zakia Menghji, Nafasi hiyo sasa imechukuliwa na Dk. Frank George Haule, ambaye ameteuliwa na Dk. Magufuli na wajumbe kuridhia katika mkutano huo
 Baashi ya wageni waalikwa wakiwemo mabalozi kutoka nchi mbalimbali
 Katibu NEC Itikadi na uenezi, Humphrey Polepole akihamasisha wajumbe wakati wa mkutano huo
 Baadhi ya wajume na waalikwa wakiwa wamesimama wakati Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akiingia ukumbini
 Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli (kushoto) akimsalimia Mke wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu John Malecela, Mama Anne Kilango Malecela baada ya kuwasili ukumbini
 Wajumbe ukumbini
 Kikundi cha ngoma za sanaa kikitumbuiza wakati wa mkutano huo
 Msanii wa kikundi hicho akionyesha umahiri wake
 Wajumbe kutoka Mara wakishangilia walipotambulishwa ukumbini wakati wa mkutano huo
 Taswira ya wajumbe na waalikwa iliivyokuwa ikionekana ukumbini
 Baadhi ya wasanii walioalikwa kwenye mkutano huo wakiwa ukumbini.
 Mke wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, Mama Janneth Magufuli akisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini
 Waziri kuu Mstaafu Mizengo Pinda akisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini
 Waziri Mkuu Mstaafu Dk Salim Ahmed Salim akisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini
 Makamu Mwenyeti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani abeid Karume akisalimia baada ya kutambulishwa
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini
 Mwenyekiti wa CCM mstaafu na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimia baada ya kutambulishwa 
 Baadhi ya wajumbe ukumbini, wapili kushoto walioketo mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme
 Wajumbe wakiwa ukumbini, Kulia ni Mama Salma Kikwete na Katibu Mwenezi Mstaafu, Waziri Nape Nnauye 
 Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli akifunga kikao hicho baada ya ajenda zote kukamilika. KWA PICHA ZAIDI YA MIA MOJA ZA TUKIO MKUTANO HUO/>BOFYA HAPA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª