Breaking News

Your Ad Spot

Mar 18, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA AFYA WA KENYA KUHUSU TANZANIA KUPELEKA MADAKTARI 500(WASIO NA AJIRA SERIKALINI) KWENDA KUFANYA KAZI NCHINI KENYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu kuhusu Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini Kenya, Ajira za Madaktari hao zitatangazwa mara moja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini  ambao hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali  waliomaliza mafunzo kwa vitendo na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Kisumu County Jack Rangumba ambaye aliambatana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyeambatana pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza jambo Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu pamoja na Gavana wa Kisumu County Jack Rangumba kabla hawajaondoka Ikulu jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza kuhusu Kutangaza ajira za Madaktari wapatao 500 ambao watakwenda kufanya kazi nchini Kenya. Ajira hizo zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali. (PICHA NA IKULU).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages