Breaking News

Your Ad Spot

Mar 10, 2017

UPELELEZI KESI YA KITILYA WASUBIRI USHAHIDI KUTOKA ULAYA



Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi Miss Tanzania wa Zamani Shose Sinare na kamishna mstaafu wa TRA, Harry Kitilya n Sioi Sumari wakiwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili

Kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya na Sioi Sumari 



Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa ndani ya nchi ya Tanzania katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umekamilika.

    Hayo yameelezwa na wakili wa Jamuhuri Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

    Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.

    Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.

     Baada ya taarifa hiyo ya upelelezi, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuwaleza upande wa jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na siyo kuleta liugha za ujanja ujanja.

   “Tunaomba upande Jamuhuri watupe majibu yenye muelekeo, waache lugha za ubabaishaji, kama upelelezi haujakamilika waseme basi siyo suala la kutueleza umekamilika ndaniya nchi lakini nje bado, haileti maana yoyote.”Amesema Magafu.

     Akijibu hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema kitendo cha kesema upelelezi wa ndani umekamilina inaonyesha kesi imepiga hatua kwa kiasi Fulani hivyo ameugiza upande wa jamuhuri ukija tena ueleze hali ya upelelezi huko nje ikoje.

    Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.

    Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

    Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.


aliyekuwa Miss Tanzania Shose Sinare akishuka katika ngazi za mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages