Katibu tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, leo amewakabidhi vyeti ya kuhitimu mafunzo ya udereva na ujasiriamali, madereva 131 wa Bodaboda katika Kata za Buguruni na Vingunguti wilayani humo.
Mafunzo hayo yaliyojikita katika nyanja mbalimbali za udereva, ambayo bodaboda hao wameyafanya kwa wiki mbili, yaliendeshwa na Kikosi cha Polisi cha Ufufundi, lakini mafunzo wamefanyika Bunguruni.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika Katika Mtaa wa Mtakuja, Buguruni, Mpogolo amewataka bodaboda hao kutumia elimu waliyopata kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa na kwa kuzingatia zaidi sheria za usalama barabarani.
Pia amewataka kutoa ushirikiano kwa Polisi na kutoa taarifa kwa uongozi wa Chama cha wamiliki na waendesha Bodaboda cha mkoa wa Dar es Salaam, wanapokamatwa huku wakiwa wanaamini kuwa wamekamatwa kinyume na utaratibu.
Amewatataka wale waliopewa kazi ya kukamata bodaboda zinazoingia mjini, kutumia weledi badala ya kuvamia waendesha bodaboda kama ambavyo imekuwa ikifanyika, kwa kuwa kufanya hivyo kunahatarisha usalama.
Aidha, amewataka bodaboda hao kutoa taarifa, pindi watakapokamatwa na kutozwa faini bila kupewa stakabadhi, kwa kuwa wanaofanya hivyo wanaikosesha serikali mapato kwa kujinufaisha wenyewe.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kushoto) akimskiliza kwa makini, Mwenyekitiwa Chama Cha Wamiliki na Waendesha Bodaboda mkoa wa Dar es Salaam, Michael Masawe, wakati kabla ya kukabidhi vyeti kwa waendesha bodaboda waliohitimu mafunzo ya fani hiyo na ujasiriamali, katika Kata ya Buguruni, leo. Pia alizindua uongozi wa Chama hicho katika Kata hiyo.
Mwenyekiti wa Waendesha bodaboda Wilaya ya Temeke akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Katibu wa Chama hicho cha Waendesha Bodaboda mkoa wa Dar es Salaam, Daudi Raurian akizungumza wakati wa hafla hiyo
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omari Kumbilamoto, akizungumza wakati wa hafla hiyo na kuomba Halmashauri ya Jijini iwaruhusu waendesha Bodaboda wa Buguruni wafike kushusha abiria Mnazi Mmoja.
Waedesha Bodaboda wakishangilia wakati wa hafla hiyo
Kumbilamoto akimkaribisha Mpogolo kuzungumza kwenye hafla hiyo
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mpogolo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodaboda Kata ya Buguruni baada ya kuzindua uongozi huo
Mpogolo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodaboda Kata ya Buguruni baada ya kuzindua uongozi huo
Vingunguti🔻
















































No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269