Breaking News

Your Ad Spot

Apr 5, 2017

DKT. SHEIN AZINDUA KITUO KIPYA CHA UNUNUZI WA KARAFUU (ZSTC) HUKO PEMBA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipokuwa akikata utepe kuzindua Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha ununuzi wa karafuu katika Kijiji cha Mgelema jana Aprili 4, 2017, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la ZSTC Dkt. Said Seif Mzee.(PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Miundombinu Ndugu, Mustafa Aboud Jumbe alipotembelea ujenzi wa Barabara ya Ole-Kengeja mpaka Ole Muhogoni Kiziwamaji, akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kijijini cha Mgelema Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba jana wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha Ununuzi wa karafuu kijijini hapo akiwa katika ziara ya kikazi

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Bw.Bakari Haji Bakari akitoa maelezo ya Kitaalam kuhusu ujenzi wa Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha ununuzi wa karafuu katika Kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chakechake  Mkoa wa Kusini Pemba, mara baada ya kuzinduliwa rasmi jana April 04/04/2017 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kijijini cha Ngomeni Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba jana wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha Ununuzi wa karafuu kijijini akiwa katika ziara ya kikazi

Baadhi ya Mawaziri na Viongozi wengine waliohudhuria katika uzinduzi wa kituo kipya cha Shirika la ZSTC cha ununuzi wa karafuu katika Kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba,wakimsikiliza Waziri wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuzungumza na Wananchi Kijijini hapo jana akiwa katika ziara ya kikazi.


  Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, kuzungumza na Wananchi wa Kijijini cha Ngomeni Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba leo wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha Ununuzi wa karafuu

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages