Mahakama nchini Zambia leo imekataa kufuta mashitaka ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani, Hakainde Hichilema, kesi ambayo imezusha wasiwasi wa kisiasa miezi kadhaa baada ya uchaguzi nchini humo uliobishaniwa.
Kiongozi huyo wa chama cha United Party for National Development (UPND) alikamatwa katika msako wa polisi nyumbani kwake mwezi huu na alifunguliwa mashitaka ya kujaribu kuipindua serikali baada ya kufikishwa katika mahakama kuu.
Mawakili wa Hichilema wamekata rufaa, wakisema madai hayo hayaeleweki, lakini jaji Greenwell Malumani aliiambia Mahakama iliyokuwa imejaa watu kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kufuta madai hayo na kuipeleka kesi hiyo katika mahakama kuu.
Zambia ilikuwa moja kati ya nchi zenye utulivu mkubwa katika eneo la kusini mwa Afrika hadi pale mahusiano yalipoharibika kati ya serikali na upinzani mwezi Agosti, wakati chama cha Rais Edgar Lungu cha Patriotic Front kukishinda chama cha UPND katika uchaguzi ulioelezwa kugubikwa na machafuko.
Source: Reuters/R. Ward
Your Ad Spot
Apr 27, 2017
Home
Unlabelled
KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI ZAMBIA KUFUNGWA JELA AU KUNYONGWA
KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI ZAMBIA KUFUNGWA JELA AU KUNYONGWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269