
Askari
polisi saba waliokuwa katika doria kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya
za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani nchini Tanzania wanadaiwa kuuawa kwa
kupigwa risasi usiku wa Aprili 13,2017.
Mkuu wa
jeshi la polisi Tanzania IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kuongeza kuwa taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa
polisi mkoa wa Pwani.
Taarifa
zinasema kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka
kwenye doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.
Imeelezwa
kuwa majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari
na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha
kutokomea kusikojulikana na kwamba silaha zote walizokuwa nazo (SMG)
zilichukuliwa na watu hao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269