Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI.
Na Khamisi Mussa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI Dkt, Respicious Boniface
amefanya mikutano na Watumishi wa MOI Dar es Salaam jana kwa makundi
kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza changamoto mbalimbali
zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi
Dkt,
Boniface amekutana na Watumishi wa idara ya utumishi ,Uuguzi na ufundi.
ambapo amewapongeza kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na
alikutana na watumishi wa idara ya Tiba Kwa upande wao Watumishi
wamempongeza Dkt, Boniface kwa kuaminiwa na kupewa dhamana ya kuiongoza
Taasisi ya MOI
Aidha,
Dkt Boniface amewaomba Watumishi wa MOI kumpa ushirikiano kwa kutimiza
wajibu na kufanya kazi kwa bidii ambapo aliwaeleza kwamba changamoto
zilizotolewa atazifanyia kazi na kuzishughulikia
“Nafahamu
changamoto ni nyingi sana, nawaahidi kuzishughulikia kama si zote basi
kwa asilimia kubwa , lengo ni kuhakikisha Taasisi yetu ya MOI inasonga
mbele na inaendelea kutoa huduma bora’’
Awali
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,wazee na watoto Mh Ummy
Mwalimu (MB) alimteua Dkt Lespicious L. Boniface kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) , uteuzi huo
ulianza tarehe 5/04/2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili MOI, Dokt. Respicious
Boniface (kushoto) akiandika jambo wakati wa Mkutano na Wafanyakazi wa
Taasisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha, kuanzia kulia ni Mkurugenzi wa
Uuguzi wa Taasisi hiyo, Flora Kimaro na Meneja Uhusiano na Ustawi wa
Jamii wa Taasisi hiyo, Jumaa Almasi
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili MOI, Dokt. Respicious Boniface akizungumza jambo katika Mkutano na wafanyakazi wa Taasisi hiyo Dar es Salaam jana
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza kwa umakini
Mfanyakazi
wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu MOI, Tula Gadi
akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Mkurugenzi Mtemdaji wa Taasisi
hiyo alipokuwa akizungumza nao kwa lengo la kujitambulisha kwao
Mmoja
wa wafanyakazi , Fidelis Minja akizungumza jamo wakati wa Mkutano wa
Mkurugenzi Mtendaji na wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI
Wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba wakiwa katika Mkutano huo
Mmoja
wa wafanyakazi Bahati Mrema akizungumza katika Mkutano huo Dar es
Salaam jana. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269