.

NAPE AFANYA KIKAO NA WAZEE MAARUFU KATIKA JIMBO LA MTAMA

Apr 15, 2017

Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye akiwasili katika kikao chake na Wazee Maarufu wa Kata za Mtama na Majengo A, kikilchofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki kijiji cha Majengo A huku akiwa ameongozana na Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Lindi Vijijini Shaibu Bakari Ngatiche .
Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye akizungumza na Wazee maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A ,katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa kaniasa la Katoliki, Mtama Lindi Vijijini. Nape alizungumza mambo mengi ikiwemo kuwaomba Wana Mtama kusameheana kwa mambo yote mabaya yaliyokuwa yametokea na kuanza ukurasa mpya wa kujenga undugu wa kupendana na kushirikiana katika mampo mbalimbali, amewaomba kuziweka kando itikadi zao za kisiasa na badala yake wakae kwa umoja wao wafikirie namna ya kuliletea maendeleo jimbo la Mtama.

"Ndugu zangu, Wazee Wangu siasa kwa sasa zimekwisha, niwaombe tu, itikadi zetu za kisiasa tulizokuwa nazo tuziweke kando, tuanze upya kwa pamoja kuijenga Mtama yetu ili ipige hatua katika suala zima la Maendeleo, na mie kwa vile nimepata nafasi ya kuhakikisha jimbo la Mtama linapata maendeleo, basi nitahakikisha yale yote niliyo yaahidi wakati wa kampeni, ndani ya miaka mitano niwe nimemaliza ama kuyapunguza kwa kiasi kikubwa", alisema Nape. 
 Baadhi ya wazee wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali ya kuhakikisha jimbo la Mtama na kusini kwa ujumla inaanza kupiga hatua kimaendeleo
 Baadhi ya kina Mama waliofika kumsikiliza Mbunge wao
 Mwananchi wa jimbo la Mtama akielezea moja ya changamoto ndani ya jimbo hilo,ambalo amemuomba Nape alifanyie kazi
Nape akiwa katikati ya Wazee Maarufu wa jimbo la Mtama wakisubiri chakula cha pamoja
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi vijijini Mohamed Nanyali akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo hilo Nape Nnauye ili kuzungumza na wapiga kura wake kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Wazee maarufu wa jimbo hilo. Picha na Michuzi Jr.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช