Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao ili kufikia malengo walioyanayo nchini.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri8 ya Muungano waq Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es salaam.
“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa anaunga mkono uamuzi wa Rais wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli kwa kutoa elimu bure nchini kwani kunaongeza idadi ya watoto wa kike kuwepo mashuleni tofauti na kipindi cha nyuma.
Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi kuwahamasisha watoto wao wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kukuza rasilimali watu katika kujenga uchumi unaotokana na viwanda nchini.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William Anangisye amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
Your Ad Spot
Apr 27, 2017
Home
Unlabelled
SERIKALI: WANAOPATA MIMBA MASOMONI KURUDI SHULENI
SERIKALI: WANAOPATA MIMBA MASOMONI KURUDI SHULENI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269