Breaking News

Your Ad Spot

May 6, 2017

ATCL KUPATA NDEGE MPYA MWEZI UJAO

Na Tiganya Vincent
Serikali imesema kuwa mwezi Julai mwaka huu (2017)itanunua ndege nyingine mpya aina ya Dash 8-Q 400 kwa ajili kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania ili  liliweze kutoa kutoa huduma za usafiri wa anga katika maeneo mengi ndani na nje ya nchi.

Hatua hiyo itaiweza ATCL kufikisha ndege nne (4) ambapo itaiwezesha kuongeza safari zake kwa kuhudumia masoko yake ya ndani na  miji ya nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Burundi , Rwanda, Malawi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano Mhandisi Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Safiri za Ndege za Shirika la ATCL mkoani Tabora.

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa hadi kufikia Julai mwakani (2018)Shirika la Ndege hapa nchini linakuwa na uwezo wa kumiliki Ndege sita zenye uwezo wa kubeba abira kwa kiwango tofauti tofauti na kusafiri mikoa mingi hapa nchi na nje ya Tanzania.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa hadi hivi sasa , serikali imeshanunua ndege mbili  aina ya Bombardier Dash 8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.

Alisema kuwa hatua inayofuata ni ununuzi wa ndege nyingine tatu aina ya  Bombardier Dash 8-Q400  ambayo itakuwa na uwezo kubeba abiria 76, CS 300 mbili zitakazobeba abiria 132 kila moja na Boeing 787 (Dreanliner ) itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 262.
Aidha ,Mhe. Ngonyani alisema kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha inaimarisha viwanja vya ndege kwa kukarabati miundombinu na kuboresha mifumo mbalimbali ya huduma za usafiri wa anga.
Alisema kuwa hatua hiyo inaenda sanjari uimarishaji wa Shirika la Ndege hapa  nchini na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege katika mikoa ambayo haina viwanja hivyo kwa sasa.
Mhe. Ngonyani alisema kuwa Serikali kupitia Shirika lake imekusudia kuhakikisha kuwa mikoa yote hapa nchini inaunganisha na usafiri wa anga.

Alitoa wito kwa kwa wananchi kutumia usafiri wa anga hasa wa Shirika hilo kama huduma ya kawaida na ya kuongeza fursa ya kibiashara kwa ajili kuimarisha  kipato kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.

Mhe. Ngonyani aliwaomba wakazi wa Tabora na maeneo mengine hapa nchini kutumia huduma za usafiri wa anga katika kutanua wigo wa biashara zao na kuhamasisha utalii na kuimarisa sekta ya kilimo cha kisasa hapa nchini.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho alisema kuwa Shirika la Ndege hapa nchini linatoa huduma nafuu ukilinganisha na mashirika mengine yanayotoa huduma hiyo hapa nchini.

Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia usafiri huo na kutokuwa wa watu wachache kama yalivyo mashirika mengine hapa nchini.

Dkt. Chamuriho alisema kuwa Shirika hilo linatoza gharama nafuu ukilinganisha na Kampuni nyingine zinazotoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini.

Alisema kuwa hivi sasa kutoka Dar es salaam kwenda Tabora kwa safari mmoja ni shilingi 330,000/- na kutoka Tabora kwenda Dodoma ni shilingi 250,000/-.

Dkt. Chamuriho aliongeza kuwa safari ya kwenda na kurudi kutoka Dar es salaam kwenda Tabora kwa safari mmoja ni shilingi 499,000/- na kutoka Tabora kwenda Dodoma ni shilingi 380,000/-

Nao wabunge wa Mkoa wa Tabora na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemshuru Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahidi yake kwa vitendo kwa kuanza kiliimarisha upya Sherika la Ndege hapa nchini.

Waliomba Serikali kupitia Shirika la ATCL kuendelea kupunza nauli za usafiri wa ndege ili wananchi wengi waweze kutumia usafiri wa anga hasa kupitia Shirika lao.
Wamesema kuwa haitakuwa na maana kama nauli zitakuwa juu na wananchi kuona usafiri wa anga ni watu matajiri tu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ametoa wito kwa wawekeza popote ndani na nje ya nchi kwenda mkoani humo kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo kufuatia kuimarika kwa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga, barabara na mawasiliano ya simu.

Alisema kuwa Tabora inayoa ardhi nzuri inayokubali ufugaji na ukilima wa mazao mbalimbali kama vile tumbaku, mahindi, alizeti mbunga, karanga miazi, mihogo na mengine mengine hatu inayowezo kuwawezesha kufunga viwanda vidogo na vikubwa.

Kwa mujibu wa ratiba ya safari za ndege za Shirika hilo mkoani Tabora zitakuwa Jumatau, Jumatano Ijumaa na Jumapili.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages