Breaking News

Your Ad Spot

May 1, 2017

HALMASHAURI TABORA ZAPEWA SIKU MBILI KUWALIPA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA JANA

Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
Serikali ya Mkoa wa Tabora imetoa siku mbili kwa Halmashauri tatu za Mkoa huo kuhakikisha wanatimitiza ahadi zao za kuwalipa fedha au kutoa zawadi kwa wanyakazi bora waliochaguliwa katika kilele cha sherehe za mwaka 2016.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa kilele cha sherehe za Mei Mosi kwa ngazi ya Mkoa huo.

Hatua hiyo ya Mkuu wa Mkoa imefuatia malalamiko yalitolewa kuhusu Halmashauri ya Igunga, Nzega Mjini na Manispaa ya Tabora kutowalipa wafanyakazi bora waliochaguliwa mwaka 2016 wakati Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) liliposoma risala yake.

Alisema kuwa ni vema Halmashauri zilizolalamikiwa zikatimiza ahadi hizo kwa kuwa ni haki ya watumishi waliofanya vizuri ili kuwahamasisha waendelee kufanya vizuri na wenzao waweze kuiga kwa ajili ya kuongeza ufanisi sehemu zao za kazi.

Bw. Mwanri aliwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zilizotajwa kuhakikisha zinawapa zawadi au kuwaandikia hundi washindi wa mwaka jana katika maeneo yao na kuwalisha Ofisini kwake taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo ifikapo Jumatano asubuhi.

Alisema kuwa hawezi kukubali Watendaji wawakatishe tamaa wafanyakazi wanaojituma na kuwajibika kwa bidii zote katika maeneo yao ya kazi na kuongeza kuwa ni vema wakapewa haki yao kama ilivyokubalika na kwa mujibu wa taratibu.

Katika risala yake TUCTA ilizitaja Halmashauri ya Nzega Mjini , Igunga, Manispaa ya Tabora na Bodi ya Tumbaku Tanzania kuwalipa zawadi wafanyakazi bora wa mwaka 2016 licha ya kuwaahidi.
Ilisema kuwa hali hiyo ni ubabaishaji na inakatisha tama kwa wafanyakazi wa meneo hayo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora awaagiza kuhakikisha wanawalipa haki zao zote watumishi wanapohamisha kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine kama kanuni na taratibu zinavyotaka.

Alisema kuwa mtumishi anapoahamishwa anapaswa kulipwa hela ya usumbufu na mwajiri wake wa awali na fedha za kujikimu yeye na familia yake na mwajiri wake mpya.

Bw. Mwanri alisema kuwa utekelezaji huo hauhitaji kiongozi juu ndiye aje kufuatilia bali ni jukumu la Wakurugenzi kuhakikisha watekelezaji taratibu hizo ili kuondoa kero sizo za lazima kwa watumishi hadi walalamike.

Maadhimisho ya Mei Mosi Kimkoa yamefanyika katika Manispaa ya Tabora ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni Uchumi wa Viwanda Uzingatie Haki , Masilahi na Hershima ya Wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages