Breaking News

Your Ad Spot

May 12, 2017

JARIBIO LA KUTAKA KUMUUA KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI NI TANGAZO LA VITA

Korea Kaskazini imelaani tena jaribio la kutaka kumuua kiongozi wake ambalo limetekelezwa mashirika ya kijasusi ya Marekani na Korea Kusini na kulitaja jaribio hilo kuwa sawa na tangazo la vita.

Katika taarifa, Ubalozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kusema nchi yake itaanza oparesheni dhidi ya magaidi ambao walihusika na njama ya kutoka kumuua kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

Taarifa hiyo imesema Pyongyang ina azma imara ya kuwasaka bila huruma na kuwaangamiza magaidi wote wa shirika kuu la kijasusi la Marekani CIA na shirika la kijasusi la Korea Kusini waliohusika na njama hiyo.

Taarifa hiyo imetoa wito kwa nchi za Umoja wa Mataifa kuunga mkono jitahada za Korea Kaskazini katika kukabiliana na magaidi hao waliotumwa na CIA.

Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilitoa taarifa na kusema kuwa, CIA na Idara ya Intelijensia ya Korea Kusini zinapanga kutumia silaha ya kemikali kumuua kiongozi wa nchi hiyo.

Haya yanajiri katika hali ambayo, hali ya taharuki ingali imetanda katika Peninsula ya Korea haswa baada ya Marekani kufanyia majaribio kombora lake la "Minuteman III" lenye uwezo wa kupiga umbali wa karibu kilomita elfu sita na 760.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages