Breaking News

Your Ad Spot

May 18, 2017

KOSA LA KUDANDIA TRENI WAKATI MILANGO IMEFUNGWA NI KIFUNGO CHA MIEZI SITA JELA

Watumiaji wa huduma za usafiri wa treni za abiria za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wametakiwa  kuzingatia  sheria za matumizi ya usafiri huo ili kuepuka adhabu ya kufungwa jela miezi sita.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka uongozi wa TRL umeainisha kuwa matumizi ya usafri wa abiria unasimamiwa na sheria , kanuni ,taratibu na masharti maalum. Mojawapo limetajwa  ni kutodandia mabehewa baada ya milango kufungwa.

Uongozi katika taarifa hiyo umesisitiza kuwa endapo mtu atafanya kosa hilo atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo kisiochopungua  miezi sita..

Taarifa hii  imetolewa  baada ya kuonekana  kushamiri vitendo vya kuvunja taratibu za usalama za usafiri wa treni.

Aina hii ya uvunjaji huo wa matumizi yasiyo salama mwaka jana  Agosti 03, 2016 yalisababisha  ,  mtu mmoja  kupoteza maisha baada ya kugongwa na geti la lango la kuingilia treni Stesheni. Marehemu alikuwa akinining’inia nje ya behewa wakati wa treni ya Pugu majira ya jioni ikiingia ndani ya  eneo la kituo kikuu cha Dar es Salaam..

Uongozi wa TRL umefafanua kuwa tofauti ya usafiri wa basi ni kwa vile  kondakta anaweza kusimamisha basi ili kumshusha mtu anayening’inia nje lakini kwa treni jinsi ilivyo ndefu  hilo haliwezekani kufanyika kirahisi.
.
Aidha katika taarifa  hiyo Uongozi uimetoa  wito  kwa wasafiri  na wananchi kwa jumla kufuata masharti ya usafiri wa treni za jiji hasa wale wanao tumia treni ya iendayo Pugu. Ili  kuepuka maafa na pia kuchukuliwa hatua za kisheria ambazo zitasababisha mkosaji kufungwa jela..

Wakati huo huo Kikosi cha Polisi Reli kimeanza operesheni ya kuwadhibiti abiria ambao hawataki kufuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya usafiri salama  wa treni na hasa kwa kuning’inia nje ya mabehewa wakati treni ikitembea. Aidha operesheni hiyo itahusisha kuwafikisha mbele ya sheria wasafri wote watakaokamatwa wakienda kinyume na masharti ya usalama wa  usafiri wa reli.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages