.

MWENDO KASI UDART MKOMBOZI WA ABIRIA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

May 11, 2017

Basi la Shirika la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART) likitoka eneo la Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuchukua Abiria Mei 10, 2017. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Abiria wakiingia katika Basi hilo

Baadhi ya Abiria wakiwa katika mstari kuingia katika Gari eneo la Muhimbili ambapo safari imeanza Mei 10, 2017
Baadhi ya Abiria wakipata huduma ya tiketi. 

Na Khamisi Mussa.

Safari tuliyoianzisha ya Muhimbili , tumeianzisha mahususi kwa kuwapunguzia Abiria wetu Gharama za nauli walizokuwa wakizitumia hapo awali ambapo walikuwa wakitoka Mbezi na kuja hadi Faya na kupanda Gari jingine.

 Hayo yamesemwa na Meneja huduma, Pius Ragero wakati alipokuwa akizungumza na waandishi (pichani hawapo) mara baada ya kuanza safari hiyo eneo la Muhimbili, alianza kwa kusema.

 Tumeanzsha safari hiyo la kuwapunguzia abiria wetu gharama za nauli  ambapo hapo awali . 
Abiria ilikuwa anatoka, mfano akianzia Mbezi anakuja hadi Faya nakuchukua usafiri mwingine kuja Muhimbili, sasa atatoka Kimara kwa Sh. 650 hadi faya na atapanda gari letu litokalo Gerezani 
kuja Muhimbili kwa gharama hiyohiyo.

Akianzia Kivukoni anakuja hadi faya na anapanda gari lakutokea gerezani hadi Muhimbili na akitokea Morocco anakuja hadi faya na anapanda gari la kutoka gerezani na kufika Muhimbili.

Hayo yalisemwa na Meneja Huduma, Ragero ambapo alisema, anawaomba abiria kutowa ushirikiano na kupenda huduma yetu kwani tumejipanga kikamilifu, alisema Ragero

Kwa sasa naona mapungufu hakuna na kama tiketi mtu anafika kituoni na kupata tiketi na kupanda gari letu na kuanza safari yakuelekea atakako ilimuradi abiria huyo asitoke nje ya kituo chetu.

Naye abiria aliyefika kupata huduma ya tiketi, Grece Kivugo alisema.
Anashukuru kwa wahusika julali na kuamua kuanzisha safari hii ya Muhimbili na kuona umuhimu na kutujali, ila anaomba ifahamike Hospitali ya Taifa Muhimbili ni hospitali kubwa , inapaswa barabara zinazo ingilia Muhimbili ziboreshwe na usafi ufanyike kuanzia nje,

Naye mkazi wa Tandika Juma Adam alikuwa na haya ya kusema, usafiri huu ni mzuri na bado matatizo madogo madogo bado yapo, kama unavyoona, mtu anakaa foleni unaambiwa tiketi hakuna kutokana na muitikiwa wa watu kuupokea usafifiri huo nakuona ni mkombozi kwao, alisema Adam,

Sasa inatakiwa waboreshe usafiri wawe  inatakiwa vituvyote viwe vimekamilika na inakuwa haina haja ya mtu kuhangaika kwa usafiri na kutozunguushana na tutakuwatumepata usafiri wa uhakika.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช