Breaking News

Your Ad Spot

May 10, 2017

RAIS JACOB ZUMA KUWASILI NCHINI LEO NA UJUMBE WA WATU 120

DAR ES SALAAM
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, anawasili hapa nchini Tanzania na ujumbe wa watu 120, leo saa tatu usiku, kufanya ziara ya siku mbili ya kikazi hapa Nchini.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam, Paul Makonda imesema, Rais Zuma atapokewa Raismi na Mwenyeji wake Rais Dk. John Magufuli, kesho Alhamisi saa tatu asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

"Amani, Upendo, Umoja, Mshikamano, Bidii na Juhudi za Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli vyote kwa pamoja vimekuwa nguzo na chachu ya kuwaleta wawekezaji kutoka nje ya nchi na viongozi mbalimbali kuwa na shauku ya kufika Tanzania.

Nchi ya Tanzania imepata heshima ya kupokea ugeni wa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Rais Jacob Zuma ambaye hapo tarehe 10/05/2017 saa 3 usiku akiwa na ujumbe wa watu 120 atawasili nchini kwa ziara ya siku mbili na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli." imesema taaifa ya Makonda.

Makonda amesema, ugeni huo utatanguliwa na ujumbe wa Mawaziri wasiopungua sita. Ambao wataungana na Mawaziri wetu katika kujadiliana namna gani ya kutumia fursa ili kujenga uchumi wetu na uchumi wa Afrika Kusini.

"Napenda kuwapa tahadhari wakazi wote wa maeneo ya jirani na Ikulu kuwa kutokana na tukio hilo kwa muda huo wanashauriwa kuwa katika hali ya tahadhari hasa kwa walio na magonjwa ya mshtuko", alisema Makonda.

Katika ziara hiyo marais hawa wawili pamoja na mambo mengine watasaini Hati mbalimbali za makubaliano ikiwemo za ushirikiano katika sekta ya maji baina ya nchi mbili hizi, ushirikiano katika sekta ya uchukuzi na katika masuala ya Rasilimali ya Wanyama na Misitu.

Kama ilivyo kawaida yetu kwa Amani, Upendo, Furaha na Ukarimu tuliokuwa nao katika kuwapokea wageni wetu tuungane na Rais wetu siku ya Jumatano katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius K. Nyerere International Airport – Terminal 1 kuwapokea wageni wetu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages