Breaking News

Your Ad Spot

May 27, 2017

TAASISI YA KIMATAIFA YA JTFE YATOA ELIMU MASUALA YA UALBINO KWA VIONGOZI WA KANISA LA KKKT - DKMZV


Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) inayojishughulisha na masuala ya watu wenye Ualbino yenye makao makuu yake nchini Uholanzi leo imetoa elimu kuhusu mambo ya ualbino kwa viongozi Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (DKMZV).
 

Taasisi hiyo imetoa elimu hiyo leo Ijumaa May 25,2017 na Mwenyekiti wa JTFE, Pieter Staadegaard kutoka nchini Uholanzi na Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka JTFE Josephat Torner anayeishi nchini Tanzania wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano kanisa la KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho,Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard alisema lengo la taasisi hiyo kushughulika na mambo mbalimbali yanayohusu watu wenye ualbino ndani na nje ya Tanzania.

Staadegaard ambaye anaishi na mtoto mwenye ualbino alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kushiriki kikamilifu katika kutokomeza vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye ualbino kwani ni vitendo ambayo vinamchukiza hata mwenyezi mungu.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka JTFE Josephat Torner alisema kutokana na vitendo wanavyofanyiwa watu wenye ualbino,vita hiyo inatakiwa kumalizwa kiimani kwani mambo ya kishirikina hayawezi kumalizwa kwa mitutu ya bunduki bali watu kubadilika kifikra.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala alisema kanisa hilo liko mstari wa mbele katika kupiga vita ukatili wanaofanyiwa watu wenye ualbino na tayari walishaunda idara maalum kwa ajili ya kushughulikia masuala hayo.
Habari katika Picha
 Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akimtambulisha Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard (kushoto) kwa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria  -Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akizungumza katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akizungumza kwa lugha ya Kiingereza huku Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akitafsiri kwa lugha ya Kiswahili
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akisisitiza jambo
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akielezea umuhimu wa viongozi wa dini kushiriki katika vita dhidi ya ukatili wanaofanyiwa watu wenye ualbino
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria  
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza.Kushoto ni Katibu Mkuu wa kanisa hilo Daniel Mono,Kulia ni Msaidizi wa Askofu kanisa hilo,Trafaina Nkya
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza jinsi kanisa hilo linaendelea na vita dhidi ya vitendo dhidi ya watu wenye ualbino
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza
Wajumbe wakifurahia jambo
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala alisema kanisa hilo limekuwa mstari wa mbele katika vitendo vya kupiga vita ukatili dhidi ya watu wenye ualbino
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akiagana na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akiagana na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akiagana na Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Trafaina Nkya

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akiagana na Katibu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Daniel Mono.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages