Breaking News

Your Ad Spot

May 13, 2017

TRA WATOA SEMINA YA MASUALA YA KODI KWA WANAHABARI TANZANIA

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo akizungumza kwenye Semina ya masuala ya kodi kwa wanahabari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kufanyika katika ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Kodi Mkuu wa TRA, Sydney Mkamba na Anjela Michael (kulia) Mwenyekiti wa Semina hiyo.
Ofisa Mkuu wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gabriel Mwangosi (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada katika Semina ya masuala ya kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika Semina ya masuala ya kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kufanyika katika ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam.

Semina ya masuala ya kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiendelea.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika Semina ya masuala ya kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kufanyika katika ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika Semina ya masuala ya kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kufanyika katika ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.
Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipajin kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza
“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.
“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo.
Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Hayo yamesemwa leo Mei 13, 2017 na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Bw. Richard Kayombo(pichani juu), wakati wa ufunguziwa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbin wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo.
Bwana Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chom,bo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma.
“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages