Breaking News

Your Ad Spot

Jul 30, 2017

JAMII: MUGABE A TYPICAL AFRICANITY

Typical Africanity ni nini?
Ndugu zangu,
Profesa Ayite anasema; " Ni hali ya kiongozi wa Kiafrika kuhofia kuandaa mrithi kwa hofu ya kufunikwa kisiasa". - Prof Ayite.

Hivyo basi, tunaona hapa, kuwa dhana ya balance of power inakosa maana. Na hili ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi za Kiafrika. Si kwenye uongozi wa nchi tu, hata kwenye uongozi wa vyama na taasisi.

Jana nimemwona Mugabe kwenye BBC News akiongea na vijana kijijini alikozaliwa Chinoyi. Kimsingi alikuwa anazungumza na vijana ambao wengi wao mwaka 1980 wakati Zimbabwe inapata Uhuru ama walikuwa ndio wanazaliwa au walikuwa hajawazaliwa.

Mugabe anasikika akiwaambia vijana;
" I am not leaving, I am not dying"

Mugame kama Kiongozi alishaondoka zamani, kisiasa alishakufa zamani. Anachofanya sasa ni kung'ang'ania kivuli chake. Inasikitisha.

Ona Mandela, katika uhai wake , mbali ya yeye kustaafu Urais, ameshuhudia Rais mmoja mstaafu kutoka Chama chake cha ANC. Mugabe hatarajii kuitwa ' Rais Mstaafu' maana atafia madarakani.

Kwamba tangu Aprili mwaka 1980 unaongoza nchi bila kumshuhudia Rais mwingine akiongoza nchi hiyo hiyo, nacho ni kipimo cha udhaifu wa uongozi.

Maana, kwa Zimbabwe, kuna waliozaliwa na kumkuta Mugabe madarakani, nao wamepata watoto, na watoto nao wamepata watoto na kumkukuta Mugabe madarakani.

Ni ukweli, Zimbabwe ya sasa, mbali ya Mugabe, haina Mzimbabwe mwingine yeyote mwenye uzoefu wa kuongoza dola.Typical Africanity!
Inasikitisha.
Maggid.
Iringa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages