Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiongea kwenye mkutano wa wataalamu wa magonjwa ya figo
nchini. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika kwenye Hotel ya Morena Mjini
Dodoma na kuhudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali
nchini, Wadau wa Maendeleo pamoja na wataalamu wengine kutoka nchi za
Kenya, Sudan,India pamoja na Norway
Makamu
wa Rais wa Chama cha wataalamu wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT),
Dkt. Paschal Ruggajjo akiongea dhima kubwa ya mkutano huo ni teknolojia
ya upandikizaji wa viungo nchini ili kuweza kuhudumia wagonjwa takribani
milioni 23.
Baadhi
ya Wataalamu wa magonjwa ya figo waliohudhuria mkutano huo. Mkutano huo
ni wa siku mbili ambapo watajadili dhana mbalimbali ya ugonjwa wa figo
ikiwemo kutoa elimu kwa umma ili kuweza kukabiliana na magonjwa ya figo
pamoja na upandikizaji.Tanzania imekua ikipeleka wastani wa wagonjwa
thelathini na tano(35) kwa mwaka nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza
figo na gharama ya kupandikiza nje ya nchi ikiwemo India ni shilingi
milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja ikiwemo kupandikiza, nauli pamoja na
malazi
Makamu
wa Rais wa Chama hicho Dkt. Paschal Ruggajjo (kulia) akimpa zawadi mmoja wa wataalamu wa figo ambaye
amefanya tafiti na kuwasilisha mada ya katika mkutano huo Profesa
Ainory Gesase ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Sayansi ya Tiba.
Picha
ya pamoja ya Mgeni Rasmi wa mkutano huo Dkt. Ndugulile akiwa na wataalamu
wa figo nchini pamoja na wadau wengine wa ndani ya nchi na nje ya nchi.
Naibu
Waziri wa Afya Dkt. Ndugulile (aliye vaa koti la bluu) akisalimiana na washiriki katika Mkutano huo mara baada ya
ufunguzi. alisema Serikali mgonjwa mmoja anahitaji wastani
wa shilingi za kitanzania 37,620,504 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia
gharama za kusafisha damu nchini
Mashine
za kusafisha figo(Dialysis Machine) ambazo zimefungwa kwenye hospitali
nchini. Serikali imefunga mashine katika hospitali nchini ikiwemo UDOM
(10),Hospitali ya Muhimbili (42), Hospitali ya Rufaa Mbeya(5), Hospitali
ya Rufaa Bugando (10), KCMC(10),Hospitali ya Misheni
Serian(10),Hospitali ya NSK Arusha(5),TMK(10),Regency(15),Hurbert
Kairuki(5), Aga Khan(10) na Access(10).Mashine hizo zina uwezo wa
kuhudumia wagonjwa 783 kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na
391 kwa huduma ya malipo ya papo kwa papo
Picha zote na Wizara ya Afya
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269