Breaking News

Your Ad Spot

Oct 2, 2017

IKULU: MNAPOMWALIKA RAIS MSITANGAZIE UMMA MPAKA IKULU ITHIBITISHE

IKULU, DAR ES SALAAM
Ikulu imewataka wanaomwalika Rais katika shughuli zao kutotangaza ushiriki wa kiongozi huyo mpaka wapate uthibitisho.

"Taasisi mbalimbali za umma na zisizo za umma zinazomualika Rais katika shughuli zao zinakumbushwa kutokutangaza ushiriki wa Rais katika shughuli zao mpaka zipate uthibitisho kutoka ofisi ya Rais", imesema taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo.

Taarifa hiyo imesema, inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli hatakuwa mgeni rasmi katika kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kama inavyotangazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tarehe 11 Oktoba, 2017 ambayo inatangazwa kuwa ndio siku ya kufanyika kwa kongamano hilo, Rais atakuwa na majukumu mengine ya Kitaifa kulingana na ratiba yake ya kazi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages