Breaking News

Your Ad Spot

Oct 24, 2017

TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 72 YA UMOJA WA MATAIFA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikagua  gwaride maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishuhudia zoezi la upandishaji wa bendera ya Umoja wa Mataifa wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja huo mapema hii leo jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Asasi ya Umoja wa Tanzania (UNA), Reynald Maeda, akitoa salamu za umoja huo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za umoja huo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzungumza na wageni waalikwa wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na wageni waalikwa wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa amesimama pamoja na viongozi mbalimbali kwa dakika moja ikiwa ishara ya kuwakumbuka askari wa Tanzania waliofariki wakiwa katika shughuli za ulinzi wa amani katika nchi mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wan chi mbalimbali wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages