Breaking News

Your Ad Spot

Oct 27, 2017

WAWILI WAFA MAJI KUTOKANA NA MVUA MKOANI PWANI-CHATANDA

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Miili ya watu wawili imeopolewa baada ya kuzama maji katika mvua kubwa iliyonyesha Oct 26/27 mwaka huu, Mkoani Pwani .

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Blasilus Chatanda, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio hayo alisema, Oct 27majira ya saa 2.30 asubuhi huko Mheza kata ya Pangani wilayani Kibaha, Saimon Ramadhani umri kati ya miaka 25-30 alifariki dunia baada ya kusombwa na maji.

Alisema Saimon alikuwa akijaribu kuvuka kwenye mto Mpiji uliokuwa umejaa maji kufuatia mvua hiyo .

Katika tukio jingine ,Chatanda alielezea ,majira ya saa 5 asubuhi ,mwili wa mtu aliyetambulika kwa majina ya Issa Ally (mgambo),umeokotwa huko mto Kiluvya .

Marehemu anadaiwa kuzama maji wakati akijaribu kumuokoa mtoto aliyetaka kusombwa na maji na hakuweza kuonekana hadi maji yalipopungua na kukutwa amekufa umbali wa km nne toka eneo alilozama maji .

Chatanda alisema,miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Tumbi na itakabidhiwa kwa ndugu baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari .

"Watu tuwe na tahadhari katika wakati huu wa mvua ,tusiamini maeneo yenye maji mengi " alisema Chatanda .

Jeshi la Polisi Mkoani Pwani ,limetoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari wakati wa kuvuka mito na maeneo yenye maji mengi ,katika kipindi hiki cha mvua ili kuepusha madhara yasiyo ya lazima 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages