Breaking News

Your Ad Spot

Nov 27, 2017

BAADA YA CCM KUZOA KATA 42 KATI YA 43 UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI, YAIPONGEZA CHADEMA KUAMBULIA KATA MOJA

Ndugu Poepole akizungumza leo
DAR ES SALAAM
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza Chadema kwa kuambulia walau Kata moja kati ya Kata 43 zilizokuwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika jana nchini kote.

Katika uchaguzi huo Chadema imepata ushindi katika kata ya Ibighi iliyopo Rungwe mkoani Mbeya ambapo imepata kura 1449 wakati CCM ikipata kura 1205 na CUF kura 12 tu.

Pongezi hizo zimetolwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.

"Kwa dhati kabisa, sisi kwa kuwa ni Chama cha kistaarabu tunakubali matokeo katika kata ile ambayo chama kimoja kikubwa cha upinzani kimeshinda, tunakipongeza sana chama hicho" alisema Polepole bila kukitaja chama hicho.

Baada ya kuzungumzia hatua mbalimbali ambazo uchaguzi huo wa marudio umepitia alilaani vitendo vya baadhi ya vyama vya upinzani vya kufanya fujo na kujeruhi watu katika maeneo kadhaa.

Akizungumzia ushindi wa CCM ambapo imeibuka kidedea katika Kata 23 kati ya 24, Polepole alisema, ushindi huo ni ishara kwamba sasa wananchi wameielewa vilivyo CCM na ni ishara kwamba uchaguzi mkuu ujao CCM itashinda kwa kishindo zaidi.

Yafuatayo ni matokeo kwenye kata mbalimbali kama alivyoyasoma Polepole

ORODHA YA KATA ZINAZORUDIA UCHAGUZI NOVEMBA 2017.
No.
KATA
JIMBO
KURA
1.
Morieti
Arusha Mjini
CCM- 8586
CDM- 3171

2.
Musa
Arumeru Magharibi
CCM-  2629
CDM- 1174

3.
Ambureni
Arumeru Mashariki
CCM- 2057
CDM- 1201

4.
Ngabobo
Arumeru mashariki
CCM-  820
CDM-  353

5.
Maroroni
Arumeru mashariki
CCM- 3568
CDM- 1176

6.
Leguruki
Arumeru mashariki
CCM- 3023
CDM- 287

7.
Makiba
Arumeru mashariki
CCM- 2022
CDM- 935

8.
Moita
Monduli
CCM- 1563
CDM- 1443

9.
Mbweni
Kawe
CCM- 2049
CDM- 1093
CUF-  114
SAU- 12

10.
Kijichi
Mbagala
CCM- 2658
CUF- 916
CDM 838
ACT- 416
ADC- 21
NCCR- 13

11.
Saranga
Kibamba
CCM- 6956
CDM-  3202
CUF-  118
ACT-  38

12.
Chipogolo
Kibakwe
George Simbachawene- CCM
13.
Bukwimba
Nyangwale
CCM- 1391
CDM- 809

14.
Senga
Geita Vijijini
CCM- 2407
CUF-  815

15.
Kitwiru
Iringa Mjini
CCM- 2171
CDM- 1473
CUF- 8
NCCR- 5
ACT- 4
ADC- 4
16.
Kimala
Kilolo
CCM- 1389
CDM- 905

17.
Bomambuzi
Moshi Mjini
CCM- 2854
CDM- 1992
CUF-  17
UDP-  02

18.
Mnadani
Hai
CCM- 1708
CDM- 958
NCCR- 3
ACT- 14

19.
Machame Magharibi
Hai
CCM- 1048
CDM- 595

20.
Weruweru
Hai
CCM- 1410
CDM- 706
CUF-  26

21.
Chikonji
Lindi Mjini
CCM- 1036
CUF-  1025
22.
Mnacho
Ruangwa
-CCM
23.
Nangwa
Hanang
-CCM
24.
Ibighi
Rungwe
CDM- 1449
CCM-  1205
CUF-   12

25.
Kiroka
Morogoro Kusini Mashariki
CCM- 2253
CDM- 277
CUF- 339

26.
Sofi
Malinyi
CCM- 2099
CDM- 1684
CUF-  12
ACT-  7
27.
Milongodi
Tandahimba
-CCM
28.
Reli
Mtwara Mjini
-CCM
29.
Chanikanguo
Masasi Mjini
-CCM
30.
Kijima
Misungwi
-CCM
31.
Muhandu
Nyamagana
-CCM
32.
Sumbawanga
Sumbawanga Mjini
-CCM
33.
Lukumbule
Tunduru Kusini
-CCM
34.
Kalulu
Tunduru Kaskazini
-CCM
35.
Muongozi
Mbinga Vijijini
-CCM
36.
Siuyu
Singida Mashariki
CCM- 1404
CDM- 1218

37.
Nyabubinza
Maswa Magharibi
-CCM
38.
Ndarambo
Momba
CCM- 1402
CDM- 1298

39.
Nata
Nzega Vijijini
CCM- 2000
CDM- 595
CUF- 33

40.
Muungano
Urambo
CCM- 1661
CDM- 882
ACT- 87
CUF- 45

41.
Majengo
Korogwe Mjini
CCM- 527
CDM- 385
CUF- 26
ADC- 17

42.
Lukuza
Lushoto
CCM- 1256
CDM- 694
CUF- 28

43.
Mamba
Bumbuli
CCM- 1399
CDM- 774
CUF- 38


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages