.

MWAKYEMBE: WATANZANIA JITOKEZENI KUMSHANGILIA BONDIA IBRAHIMU CLASS

Nov 13, 2017

Na Anitha Jonas WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Dk. Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kumshangilia bondia Ibrahim Class katika pambano lake la kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia kutoka Afrika ya Kusini  Koos  Sibiya.

Mwakyembe ametoa wito huo jana  jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake bondia  kwa pambano litakalofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017.

“Bondia huyo anauwezo mkubwa na amekwisha kushinda mara mbili kwa Afrika na kwa mkanda huu wa kugombea ubingwa wa dunia nimeona ni vyema akapigania hapa nchini ili watanzania waweze kuona uwezo wake na pamoja na kumongezea ari ya kupambana kwa ajili ya watanzania walikuja kumuunga mkono,”alisema Dk.Mwakyembe.

Mwakyembe alisema  atasimamia mchezo wa ngumi na kuhakikisha unarudisha heshima yake kama ilivyokuwa zamani kwa kuhakikisha anadhibiti wapiganaji wanaokwenda kwenye mapambano na kununuliwa huku wakililetea sifa mbaya taifa ya kutumika kupandisha watu madaraja.

Waziri Mwakyembe  amesema kuwa serikali itaanzisha bodi itakayosimamia sekta ya ngumi kwa lengo la kuondoa kukosekana kwa dira ya usimamizi wa sekta ya ngumi nchini

Bondia Ibrahim Class aliwahakikishia watanzania kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha anauchukua ubingwa huo na mkanda huo kubaki nchini huku akiwataka watanzania kuja kujionea wenyewe namna atakavyopambana na kuonyesha uwezo wake.

“ Nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa  waje kujionea wenyewe jinsi gani nitakavyo mpiga huyo mwafrika kusini na kuchukua mkanda nimejiandaa vizuri na mazoezi ninayofanya niyakiwango cha juu,”alisema bondia Class.

Rais wa TPBC Chaurembo Palasea alisema mchezo wa ngumi umekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ulingo kwa ajili ya kufanyia mazoezi kwani hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa sekta ya mchezo wa ngumi. 
Bondia Ibrahim Class (kulia) akifanya mazoezi na Mwalimu Msaidizi Kelvin Magembe huku Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na MichezoDkt. Harrison Mwakyembe(katikatia) akishuhudia, alipomtembelea kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi ya bondia huyo kwa pambano litakalofanyika kati yake na Bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017 Uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª