Breaking News

Your Ad Spot

Nov 19, 2017

TANZANIA: NI AIBU KUOMBA MISAADA NJE YA NCHI, JAMBO HILO LINALIDHALILISHA TAIFA

Tanzania: Ni aibu kuomba misaada nje ya nchi, jambo hilo linalidhalilisha taifa
Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Philip Mpango amesema kuwa, ni aibu kuomba misaada  nje ya nchi na kuongeza kwamba, binafsi amechoka kufanya hivyo kwa kuwa kitendo hicho kinalidhalilisha taifa.
Mpango aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi, wasimamizi na wahariri wa takwimu za mapato na matumizi binafsi katika ngazi ya kijamii. Akizungumzia suala hilo Mpango alisema: Aliweka wazi zaidi kwamba kuna udharura wa nchi kuwa na mkakati wa kuondokana na hali hiyo na kwamba, malengo hayo yatafikiwa kama makusanyo ya takwimu yatafanyika na kutumiwa kwa umakini.
Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania
Matamshi ya Waziri wa Fedha wa Tanzania ya kutofurahishwa na kitendo cha mataifa ya Afrika kuomba misaada kwa nchi za kigeni, yametolewa katika hali ambayo akthari ya nchi hizo zimekuwa tegemezi kwa misaada ya wahisani licha ya kuwa na raslimali nyingi zitokanazo na vyanzo asilia, kama vile dhahabu, mafuta, gesi na kadhalika. Aidha Rais wa Tanzania John Magufuli naye kwa mara kadhaa amekuwa akielezea utajiri mkubwa wa taifa hilo hususan madini, lakini pamoja na hayo bado utajiri huo haujaweza kuwanufaisha Watanzania kutokana na sababu tofauti kuu zaidi ya yote zikitajwa kuwa ni ufisadi wa baadhi ya viongozi wasiokuwa na uzalendo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages