Breaking News

Your Ad Spot

Nov 13, 2017

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA VYAMA VYA SIASA NA KUVITAKA KUZINGATIIA SHERIA KATIKA KUFANYA KAMPENI ZA UDIWANI

JAJI KAIJAGE
NA HUSSEIN MAKAME-NEC
Mwenyekitiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistolces Kaijage amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili ya Uchaguzi.

Jaji Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa NEC na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kuelekea Uchaguzi mdogo wa madiniwa.

Alisema iwapo ukiukwaji au uvunjaji wa Maadili  hayo utatokea, Chama au Mgombea awasilishe malalamiko hayo mbele ya Kamati husika ili ishughulikiwekisheria.

Aliwakumbusha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 53 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Tume inayo mamlaka ya kuruhusu kuwepo kwa Kampeni za Uchaguzi katika maeneo ya Uchaguzi na siyo Mikutano ya Vyama vya Siasa. 

Hivyo, kampeni hizo zifanyike kwenye Kata husika na inategemewa kuwa Mikutano ya Kampeni italenga kuwashawishi, kwa namna ya kistaarabu, wananchi wa Kata husika ili wamchague Mgombea anayefanyiwa kampeni. 

” Kwa mujibu wa kipengele cha 2.1. (c) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 tunategemea kila Chama cha Siasa kiendelee kufanya Kampeni kwa mujibu wa ratiba. Kampeni zote zinatakiwa kuanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni” alisemaJaji Kaijage.

Alisema kwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Tume imekwisha kutoa ushauri kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya ili katika kipindi hiki cha Uchaguzi wahakikishe wanazingatia wajibu wao na ukomo wa madaraka yao katika shughuli za Uchaguzi kuanzia kipindi cha Kampeni hadi kutangazwa kwa Matokeo. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani aliviomba Vyama vya Siasa kuwahimiza wanachama na wapenzi wao walioandikishwa kuwa Wapiga Kura wajitokeze  Siku ya Uchaguzi kwenda Kupiga Kura zao bila hofuyoyotekuhusu usalama wao.

“Ni imani ya Tume kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa mtakuwa chachu ya kuwaongoza na kuwaelekeza wanachama, wafuasi na mashabiki wenu katika kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu", alisema Kailima.

Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika kata 43 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika tarehe 26 Novemba, 2017 ambapo wapigakura 333,309 wanatarajiwa kupiga kura siku ya uchaguzihuo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa kwenye mkutano wa Tume na vyama hivyo jijini dare s Salaam, leo, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa wa madiwani, utakaofanyika Novemba 26, 2017.  Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages