Breaking News

Your Ad Spot

Jan 29, 2018

RAIS MAGUFULI NA MAMA JANETH MAGUFULI WATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA MAREHEMU JAJI MSTAAFU ROBERT KISANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 28, 2018 ametia saini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pia wametoa mkono wa pole kwa mke wa Marehemu Mama Maria Kisanga na kufanya maombi ya pamoja na familia ya marehemu.
Jaji Mstaafu Robert Kisanga alifariki dunia tarehe 23 Januari, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam,  Januari 28, 208.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mtoto wa marehemu, Amani Kisanga, baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Januari 28, 2018. kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma na kulia ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakifanya maombi pamoja na mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga na mtoto wa marehemu Amani Kisanga na waombolezaji wengine baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam . 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 
 Mama Janeth Magufuli akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam
 Waheshimiwa Majaji na waombolezaji wengine wakiwa kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Mstaafu Joseph sinde Warioba  baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA IKULU)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages