Breaking News

Your Ad Spot

Feb 2, 2018

RAIS DK MAGUFULI AOMBOLEZA KIFO CHA MZEE KINGUNGE KILICHOTOKEA LEO ALFAJIRI

Rais Dk. Magufuli alipoenda kumjulia hali Mzee Kingunge wakati akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

IKULU, DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha mmoja wa waasisi waTaifa na mwanasiasa mkongwe nchin iMzee Kingunge Ngombale Mwiru kilichotokea leo tarehe 02 Februari, 2018 saa 10:30 alfajiri katika Hospitali yaTaifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa wake nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Desemba, 2017.

Mhe. Rais Magufuli amesema Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye alitoa mchango mkubwa katika juhudi za kupigania uhuru na baada ya kupata uhuru akiwa mtumishi mtiifu wa Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM), na katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali.

“Mzee Kingunge Ngombale  Mwiru ametoa mchango mkubwa sana, sisi kamaTaifa hatuwezi kusahau na tutayaenzi mema yote aliyoyafanya wakati wa utumishi wake uliotukuka, ametuachia somo la kupigania maslahi ya nchi wakati wote, kuwa wazalendo wa kweli, kudumisha amani na mshikamano, kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuwa na nidhamu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kufuatia msiba huu, Mhe.Rais Magufuli amewapa pole wanafamilia wote, wanachama wa CCM, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu, na amewaombea kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages