.

MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM MKOA WA KIGOMA DK KABOUROU AFARIKI DUNIA, RAIS DK. MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

Mar 7, 2018

IKULU, DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli ametuma slama za rambirambi kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa CCM wa zamani wa mkoa wa Kigoma Dk. Walid Amani Kaborou (Pichani), kilichotokeea  usiku wa kuamkia leo, Machi 7, 2018.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imemkariri Raid Dk Magufuli akiomboleza kifo hicho kwa kuanza kusema “Kwa masikitiko nimepokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Kigoma Dk. Walid Amani Kaborou kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 07 Machi, 2018 katika Hospitali yaTaifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dk. Walid Amani Kaborou atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali  ndaniya CCM, na alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjinina Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Natoa pole kwa familia yake, wana CCM wote, wananchi waKigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msibahuu”

Rais ametuma salam hizo kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kufuatia kifo hicho Ikulu imesema pamoja na salam hizo Rais ameiomba familia ya marehemu na wote walioguswa kuwa na moyo ya subira, wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea Marehemu roho yake ikapumzike mahali pema peponi.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช