Breaking News

Your Ad Spot

Mar 13, 2018

RAIS MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI AWAMU YA PILI YA UJENZI WA RELI – IHUMWA DODOMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 14 Machi, 2018 ataweka jiwe la msingi katika sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” inayoanzia Morogoro hadi Makutupora Mkoani Dodoma.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi zitafanyika kesho kuanzia saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wananchi wa Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli hapa nchini Masanja Kadogosa anasema maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi katika sherehe hizo yamekamilika na amewataka wananchi kujitokeza katika sherehe na waliombali na Dodoma kufuatilia matangazo yatakayorushwa hewani na vituo vya redio na televisheni

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages