.

SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO NA BHART AIRTEL

Mar 12, 2018

IKULU, DAR ES SALAAM
Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza rasmi leo tarehe 12 Machi, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo kamati iliyoundwa na Rais Magufuli inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti Airtel inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wake Mukesh Bhavnani.

Mazungumzo hayo yanalengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili (Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel) na kuimarisha sekta ya mawasiliano nchini Tanzania.

Kampuni ya Bharti Airtel iliomba kufanyika kwa mazaungumzo hayo baada ya kamati iliyofanya uchunguzi kuhusu umiliki wa kampuni ya Airtel Tanzania kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Dk. John Magufuli.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช