.

RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA DK MNDOLWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BODI Y A BENKI YA TPB

Apr 23, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Dk. Edmund Bernard Mndolwa (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB).

Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema teuzi wa Dk. Mndolwa umeanza leo tarehe 23 Aprili, 2018.

Taarifa hiyo imesema Dk. Mndolwa anachukua nafasi ya Prof. Lettice Rutashobya ambaye amemaliza muda wake.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช