Breaking News

Your Ad Spot

Dec 31, 2009

SIMBA WA VITA AMEFARIKI LEO

  Marehemu, Mzee Rashiud Kawawa enzi za uhai wake  Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mzee Kawawa mapema mwaka huu.
RAIS Jakaya Kikwete akitangaza rasmi kifo cha Mzee Rashid Mfaume Kawawa leo, Ikulu, Dar es Salaam.

Stori
MWANASIASA maarufu na mkongwe Rashid Kawawa, amefariki dunia leo saa 3:20 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbuli mjini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa kisukari na figo.

Kifo hicho kilitangazwa rasmi leo na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam, akisema kifo cha Mzee Kawawa ni pigo na msiba mkubwa si tu kwa familia yake bali kwa taifa nzima, kwakuwa wakati wote wa uhai wake alijitoa kuliasisi na kuendeleza Taifa.

"Mzee Kawawa, Simba wa vita ametutoka, hatunaye tena , lakini atabaki daima katika nyoyo na fikra zetu, kwa miaka mingi, hata baada ya kustaafu uongozi aliendelea kuwa nguzo muhimu kwa taifa letu" alisema Rais Kikwete.

Kufuatia msiba huo, Rais Kikwete alitangaza kuwa Taifa litakuwa katika siku saba za maombolezo ambapo bendera ya taifa itapeperushwa nusu mlingoti nchi nzima na Watanzania watapata fursa ya kutoa salamu za mwisho uwanja wa Taifa kwa utaratibu utakaotangazwa.

Kikwete alisema Kawawa alikuwa akijiandaa safari ya nje ya nchi hivyo alikwenda kupima afya yake katika Hospitali ya Usalama wa Taifa, Kijitonyama ambapo hawakuona Malaria lakini wakiwa njiani na mkewe hali ya mzee ilibadilika ghafla nakupoteza fahamu ndipo walimpeleka Muhimbili.

"Baada ya kufikishwa hospitalini hapo, alipimwa nakugundua kuwa sukari katika mwili wake ilikuwa imepungua ndipo akaongezewa maji maalumu kupandishi hali hiyo na alipata nafuu, leo saa 12 asubuhi hali ilibadilika ghafla madakatari wakabaini kuwa sukari imekauka tena na figo zake zote mbili zimeacha kufanya kazi, wakaanza jitihada kusaidia maisha yake lakini pia wakagundua na moyo wake umeshindwa kufanya kazi, hatimaye saa 3:20 Mungu akapitisha uamuzi wake" alisema Rais Kikwete.

Mapema, Daktari bingwa wa magonjwa mahutiti Dk. Mpoki Ulisubisya, aliyekuwa akimtibu hospitalini hapo, alisema Kawawa alifikishwa hospitalini hapo saa 10 za jioni ya janai, akisumbuliwa na sukari na figo. baada ya kumtibu alipata nafuu na alikuwa akiendelea vizuri japo bado alikiwa chini ya uangalizi katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) kutokana na hali yake kubadilika badilika ambapo jana asubuhi aliamka vizuri na alikuwa anatambua watu. Mwili utaagwa rasmi leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
                        
PICHA ZAIDI.........

MZEE Kawawa akiwa  mgeni rasmi kwenye shindano la Miss Tanzania ambalo mshindi aliyeibuka Richa Adhia. Shindano hil;o lilifanyika katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

MZEE Kawawa akaiwa na Mwalimu Nyerere, Rais Wa Zanzibae Aboud Jumbe enzi hizo katika moja ya hafla za kitaifa. pembeni ni Samora Machel aliyekuwa rais wa Msumjibi.



MZEE Kawawa akiungana na viongozi wengie akiwemo Mwalimu Nyrere  katika sherehe ya Uhuru wa Tanganyika.
MZEE Kawawa na Mwalimu Nyerere wakiwa na Kiongozi wa  Dhehebu la Ismailia Duniani HH The Agakhan.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages