Breaking News

Your Ad Spot

Jan 7, 2010

IVORY COAST YAMALIZA ZIARA BONGO KWA KUINYUKA RWANDA 2-0

MGWNI rasmi, Waziri Kiongozi mstaafu, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akikagua wachezaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast,The Elephants, kabla ya mechi ya kirafiki ya Kimataifa kati ya timu hiyo na timu ya Taifa ya Rwanada, Amavubi, jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kushoto ni Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba. 
Kikosi cha Ze Tembo ya Ivory Coast
Kikosi cha Amavubo ya Rwanda
Mashabiki  waliohuhudia mtanange huo
MSHAMBULIAJI ambaye pia ni Nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coas, The Elephants, Didier Drogba (kushoto) akivuta mpira dhidi ya beki wa timu ya Taifa ya Rwanda, Amavubi timu hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Didie Drogba akiwaaga mashabiki baada ya mechi, huku akilindwa na baunsa wake.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Ivory Coast maarufu kama  Za Tembo Vahid Halilhodzic wa Bosnia, akimkubatia na kumnong'oneza jambo Nahodha wa timu hiyo Diodier Drogbar baada ya mechi.

                                                          

                                                                    STORI
TIMU ya Taifa ya Ivory Coast yaani The Elephants au Matembo leo wameliza ziara yao hapa Bongo kwa kuikung'uta Amavubi ya Taifa la rwanda mbili bila.

Walikuwa nchini kwa michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa, ikijinoa kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zinazoanza kutimua vumbi mwisho wa wiki hii nchini Angola.

Licha ya ushindi huo, Ivory Coast Rwanda nayo kama Stars ilikomaaa kiaina kwa kuonyesha kiwango kizuri cha soka na kuwatoa jasho wachezaji wa timu hiyo.

Katika mchezo huo, Ivory Coast ilianza mchezo kwa kasi, ikionekana kukamia kutafuta mabao mapema, lakini uimara wa mabeki wa Rwanda uliifanya timu hiyo kushindwa kufurukuta.

Sekunde chache baada ya mchezo kuanza, timu hiyo yenye wachezaji karibu wote wa kulipwa wanaocheza soka nje ya nchi yao, akiwemo Didier Drogba, ilifanya shambulizi kali langoni kwa wapinzani wao, lakini kipa Jean Claude Ndoli wa Rwanda, aliondoa hatari hiyo langoni mwake.

Dakika ya nne, Ivory Coast ilipata tena nafasi kupitia kwa Bakari Kone, aliyebaki pekee na kipa, lakini mpira aliopiga ulipanguliwa na kipa huyo kabla ya mabeki wake kuondosha mpira katika eneo la hatari.

Ivory Coast iliendelea kufanya mashambulizi na dakika ya 10 Drogba alipata tena nafasi, baada ya kupokea pasi safi ya Kouassi Gervas, lakini mpira aliopiga ulipaa na kutoka nje.

Rwanda ilijitahidi kufurukuta na kutandaza kandanda safi ilipopata nafasi, na dakika ya 21 Yusuf Ndayishimiye alipata nafasi lakini shuti hafifu alilopiga liliokolewa na kipa Barry Boubakar.

Laiti kama Drogba asingekuwa akicheza kwa kukamia katika mchezo huo, angeweza kupatia timu yake mabao mengi, baada ya kupata nafasi nyingi za kufunga, lakini mipira aliyopiga ilipotelea hewani.

Drogba ambaye ni kapteni wa timu hiyo, alipata nafasi za wazi dakika za 22 na 28, kabla ya Bakari Kone na Kouassi Gervas kupata nafasi zingine za wazi dakika za 35 na 44, lakini zote hazikuzaa matunda.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana, na kipindi cha pili kilipoanza timu zote zilianza mchezo kwa kasi.

Drogba aliyekuwa akihaha kuitafutia mabao timu yake, alianza tena kipindi hicho kwa kucheza kwa kasi na dakika ya 55 na 60 alipata tena nafasi za kufunga, lakini golikipa Jean Luc Ndayishimiye, aliyeingia kipindi cha pili, alikuwa kikwazo kikubwa kwa washambuliaji wa Ivory Coast.

Rwanda ilijibu mashambulizi ya mchezaji huyo dakika ya 63 na 65 baada ya kupata nafasi za wazi, lakini umaliziaji mbovu uliifanya timu hiyo kuangukia pua na kushindwa kupata hata bao la kufutia machozi licha ya kutandaza kandanda safi.

Ivory Coast iliandika bao lake la kwanza dakika ya 86 kupitia kwa Suleyman Bamba, aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi baada ya kuunganisha mpira wa kona uliopigwa kutoka mashariki ya uwanja.

Baada ya bao hilo Ivory Coast ilizidisha mashambulizi, na dakika mbili baadae Solomon Kalou, aliiongezea bao la pili baada ya kuwakimbiza mabeki wa Rwanda na kuachia shuti kali lililojaa moja kwa moja wavuni.

Ivory Coast iliwachezesha Barry Boubakar, Emmanuel Eboue/Angoua Brou, Kolo Toure, Abdulaye Meite/Kader Keita, Siaka Tiene, Kuomatiene Kone/Suleyman Bamba, Tiote Cheick/Jean Gosso, Didier Zokora, Bakari Kone Solomon Kalou, Didie Drogba/Haruna Dindane na Kouassi Gervas/Yaya Toure.

Rwanda: Jean Claude Ndoli/Jean Luc Ndayishimiye, Didier Kapet, Aman Uwiringimana, Donatien Tuyizere, Eric Gasana, Mutesa Mafisango, Jamal Mwiseneza, Haruna Niyonzima/Jean Iranzi, Jean Baptiste, Abbas Rassou na Yussuph Ndayishimiye.

Ciao.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages