MENEJA wa Programu wa Mfuko wa Waandishi wa Habari (TMF), Ernest Sungura akizungumza na Waandishi wa habari, jana kwenye ofisi za mfuko huo, mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa (TMF) Marjan Besuijen.
HABARI KWA UFUPI
MFUKO wa Vyombo vya Habari (TMF) umewataka Waandishi wa habari kuchangamkia fursa ya kuomba ruzuku kwenye mfuko huo kwa ajili ya kuandika habari zenye maslahi kwa umma.Hayo yalisemwa na Meneja wa programu wa mfuko huo, Ernest Sungura alipokuwa akitangaza kuanza kwa utoaji wa ruzuku hizo kwa mwaka huu wa 2010.
Alisema, mfuko huo umejiweka bayana kwamba lengo lake kubwa ni kutaka ziweze kuandikwa kwa kina cha kutosha habari zenye kuimarisha misingi na utawala bora na zenye kuanzisha mijadala kwa manufaa ya umma.
Alisema, kama ilivyokuwa mwaka jana, TMF imetenga kiasi cha sh. bilini 2.1 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa wandishi wa habari watakaoomba na maombi yao kufanikiwa kupitishwa kutokana na vigezo vilivyowekwa.
Sungura alisema, katika maombi mwandishi anatakiwa kuwasilisha wazo la habari ambalo uzito wake utaonekana kuwa unastahili kufanyiwa kazi.
Alisema, habari zinastostahili mwandishi kupatiwa ruzuku ni za aina mbili ambazo alisema, ni zile za uharaka ambazo zikipofanyiwakazi zinakoma kuwa habari na zile ambazo zinamguzo lakini zinastahili kuandikwa kwakina licha ya kwamba ni endelevu.
Sungura alisema, mwaka jana karibu waandishi 150 walijitokeza na kupata ruzuku na wengi wao walionyesha kufanya vizuri ambapo habari walizofuatilia zilizaa matunda ikiwemo kutoa msukumo wa uwajibikaji.
Hata hivyo, alisema waliojitokeza kuomba ruzuku ni waandishi wa habari wa magazeti lakini wa radio na televisheni walikuwa wachache huku wapigapicha wakiwa hawakujitokeza kabisa mbali na wale aliobebwa na waandishi.
Kutokana na hali hiyo, Sungura aliwataka wapigapicha na waandishi kutoka vyombo vya televisheni na radi kujitokeza kwa wingi katika awamu hii inayoanza mwezi huu wa Januari,
Alisema, kutokana na umuhimu wa kukuza uandishi wa habari za kina zinazogusa jamii na uwajibikaji, mfuko umeongeza awamu za kutoa ruzuku hadi kufikia tatu badala ya mbili zilizokuwepo.
Sungura alisema,wakati hadi kufikia mwaka jana ruzuku zilikuwa zikitolewa kila mwezi Januari na Julai kila mwaka, sasa zitatolewa pia mwezi Aprili.
cioa
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269